AV

'Jumuisha maafisa vijana kwenye jumbe za kulinda usalama'

Get monthly
e-newsletter

'Jumuisha maafisa vijana kwenye jumbe za kulinda usalama'

— Kossi Gavon mwenye umri wa miaka 24, ni Luteni kutoka Togo anayehudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Mali. (MINUSMA)
Franck Kuwonu
Afrika Upya: 
27 May 2021
Kossi Gavon, 24, is a lieutenant from Togo serving in the UN AVkeeping Mission in Mali. (MINUSMA).
Kossi Gavon mwenye umri wa miaka 24, ni Luteni kutoka Togo anayehudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Mali. (MINUSMA)

Kossi Gavon mwenye umri wa miaka 24, ni Luteni kutoka Togo anayehudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Mali. (MINUSMA). Mmoja wa walinda amani wenye umri mdogo sana, ndiye Afisa Mkuu anayesimamia ofisi ya kamanda wa kikosi cha Togo. Anasema anashukuru kwa nafasi ya kutumika na kujifunza:

Wewe ni mmoja wa walinda amani wenye umri mdogo sana katika kikosi cha Togo katika ujumbe huu nchini Mali. Je, umewezaje kutumwa?

Haikuwa chaguo la kibinafsi. Nilifika Mali kwa kazi ya kiutawala. Kama jeshi, jukumu letu ni kulinda raia na kulinda masilahi ya nchi zetu. Utulivu katika eneo ndogo la [Afrika Magharibi] ni mojawapo ya masilahi haya, na kwa kuwa kuna haja nchini Mali, wakubwa wetu waliona inafaa kututuma hapa. Wamejitolea kulete utulivu katika eneo hili ndogo, na ni kwa uzingatiaji wa hayo ambapo nilitumwa hapa.

Kuwa kijana, unahisije kuwa katika kazi hii muhimu?

Nahisi kupata hadhi ya juu. Ni muhimu kushirikisha maafisa vijana katika jumbe kama hizi.

Je, majukumu yako ya kila siku ni yapi?

Ninasimamia rasilimali watu na pia mimi ndiye Afisa Mkuu wa kamanda wa kikosi cha Togo. Ninafanya kazi na maafisa wengine, hasa katika shughuli na ujasusi. Hii inaniruhusu kupata ujuzi wa ziada, na nifaidika sana kutokana na tajriba zao.

Kuwa kijana na kufanya kazi na maafisa wakuu kunaonekana muhimu kwako. Je, ni mambo gani mawili au matatu ambayo umejifunza kutoka kwao?

Ninafanya kazi na maafisa wenye tajriba pevu zaidi waliokamilisha kozi nyingi za wafanyakazi. Nimejifunza mengi kutoka kwao, hasa katika maeneo ya kupanga na kuratibu. Kuna mambo mengi ya kufanya kabla ya kutumwa katika ujumbe, na yananisaidia kupanga kazi yangu vizuri.

Je, kuna changamoto yoyote ya kuwa kijana katika kulinda amani?

Kuwa mchanga zaidi hapa, nadhani ninachokosa zaidi ni familia yangu. Lakini naweza kukuhakikishia kuwa kuna familia ya pili inayojaza utupu huo - familia yangu ya wanajeshi hapa. Pamoja, tuna urafiki wa karibu sana.

Unahusika zaidi katika majukumu ya kiutawala. Je, huwa unaenda nyanjani na au vitani?

Ninaweza kusema kuwa kuwepo kwenye kiini cha operesheni, tuko kwenye vita kwani vituo vya Umoja wa Mataifa haviachwi nje ya mashambulio na vikundi vya jihadi. Kufanya kazi katika hali hizi, sio lazima mtu aende uwanjani kusema kwamba yuko vitani.

Kwa kawaida siku yako huwa vipi?

Kama Afisa Mkuu lazima nifuatilie ajenda ya Kanali anayeamuru kikosi, na kuhudhuria na kufuatilia kila kitu kilicho chini yake. Na kama mkuu wa rasilimali watu, ninawajibika pia kufuatilia masuala ya wafanyakazi.

Je, unahisije wakati wenzako wako nje kwenye vita, wakikabiliwa na hatari kila siku?

Kuna hisi kadhaa wakati mmoja. Nina wasiwasi wakati wenzangu wako uwanjani kwa sababu kuna tishio la kweli, lipo na huwezi kulipuuza. Lakini wanatimiza lengo lao na kurudi, wakati huo huo huwa ninaridhika kwa sababu tunatimiza wajibu wetu, ambao ni kulinda raia na kudumisha amani katika eneo tunaloliwajibikia.