¹ú²úAV

2024: Mwaka wa matumaini ya tahadhari kwa chumi za Afrika zinazokabiliwa na changamoto duniani kote

Get monthly
e-newsletter

2024: Mwaka wa matumaini ya tahadhari kwa chumi za Afrika zinazokabiliwa na changamoto duniani kote

Ukuaji wa uchumi wa bara hilo unatarajiwa kufikia hadi asilimia 3.5
Franck Kuwonu
Afrika Upya: 
4 January 2024
Betty Mtewele, a market vendor.
Photo: UN Women/Daniel Donald
Betty Mtehemu, Naibu Mwenyekiti wa Sekta ya Nguo za Vitambaa, na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika Soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam.

Huku chumi za Afrika zikitazamia mwaka mpya, nchi katika bara zima ziko tayari kupata mafanikio ya wastani ya kiuchumi lakini lazima zikabiliane na changamoto za ndani na za kimataifa.

Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Kiuchumi na Matarajio ya Dunia (WESP) 2024, ukuaji wa kiuchumi wa bara hilo unatarajiwa kuimarika kidogo, huku wastani wa Pato la Kitaifa ukiwezekana kufikia asilimia 3.5.

Ilhali, wasiwasi wa uendelevu wa deni, shinikizo la kifedha, na mabadiliko ya tabianchi yanaleta shaka.

Ukuaji unaotarajiwa wa asilimia 3.5 ni ongezeko dogo kutoka asilimia 3.3 mwaka 2023.

Chumi kubwa za kikanda kama ule wa Misri, unatarajiwa kushuka hadi asilimia 3.4 kutoka 4.2 mwaka uliotangulia, hasa kutokana na uhaba wa fedha za kigeni ambao unaweza kudhoofisha uwezo wa kuagiza bidhaa na utashi wa ndani ya nchi.

Nchini Afrika Kusini, mzozo wa nishati unaoendelea umepunguza ukuaji hadi asilimia 0.5 tu mwaka 2023, na hakuna mabadiliko makubwa yanayotarajiwa mwaka 2024.Ìý

Nchini Naijeria, matarajio ya ukuaji wa nchi yanaashiria ongezeko la wastani, hasa kutokana na mageuzi ya serikali katika sekta ya mafuta. Ukuaji huo unatabiriwa kuwa asilimia 3.1.

Mzigo wa deni

Viwango vya juu vya madeni ni mojawapo ya changamoto kuu ambazo chumi za Afrika zinakabiliana nazo katika siku za usoni, ripoti ilibainisha.

Kwa mfano, Zambia inapitia uwiano wa deni kwa Pato la Kitaifa ambao ulipanda zaidi ya asilimia 70 katika miaka ya hivi karibuni.

Ilhali, nchi hiyo haiko peke yake: "Nchi 18 barani Afrika zilirekodi uwiano wa deni kwa Pato la Kitaifa wa zaidi ya asilimia 70 mwaka 2023, huku nyingi zikikabiliwa na dhiki ya madeni," Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (UNDESA) ilisema katika taarifa inayoambatana na Ripoti hiyo.

Hali ya kifedha ya Ghana pia inachunguzwa, huku asilimia kubwa ya tano ya mapato yake ya kodi yakitolewa kulipia deni.

Matukio haya sio hitilafu bali ni uwakilishi dhahiri wa tatizo la madeni ambalo mataifa mengi ya Afrika yanakabiliana nayo.

Hali ya kifedha na mfumuko wa bei

Uthabiti wa kifedha bado haujapatikana, Ripoti ilisisitiza, huku nchi nyingi zikipambana ili kuongeza mapato yao ya kodi, njia muhimu ya uendelevu wa kiuchumi.Ìý

Marekebisho ya ruzuku ya nishati katika mataifa kama Naijeria na Angola yanaakisi majaribio ya kurekebisha sera za kifedha huku kukiwa na hali halisi ngumu ya kiuchumi.

Wakati uo huo, shinikizo la mfumuko wa bei limeenea, huku mataifa kama Naijeria na Misri yakishuhudia ongezeko kubwa la bei za vyakula.

Katika kuwajibikia, benki kuu katika bara zima zimeimarisha sera za kifedha, kujaribu kuleta uthabiti wa sarafu na kukabiliana na mfumuko wa bei.

Hata hivyo, ufanisi wa hatua hizi katika kukabiliana na mtikisiko wa uchumi wa kimataifa bado ni swali muhimu.

Mabadiliko ya tabianchi

Mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuwa kichocheo kisichotabirika, na kuathiri kwa kiasi kikubwa chumi zinazotegemea kilimo. Upembe wa Afrika mara kwa mara unakumbwa na ukame, na kudhoofisha utoshelevu wa chakula na uthabiti wa kiuchumi.

Udhaifu wa Kusini mwa AfrikaÌýulifichuliwa na Kimbunga Freddy mnamo Machi 2023, na hasara ikiongezeka hadi mamia ya mamilioni.

Matukio haya yanasisitiza hitaji la dharura la mikakati ya kustahimili tabianchi.

Biashara

Kudorora kwa biashara duniani pia kumepunguza kasi ya ukuaji wa kiuchumi barani Afrika. Hii inatokana na utashi mdogo kutoka nchi kuu zinazonunua bidhaa za Afrika na bei za malighafi na bidhaa zinazouzwa na bara hilo zimeacha kuongezeka.

Ingawa kwa ujumla biashara ya ndani ya Afŕika inasalia kuwa chini kiasi katika bara zima, ikiwa chini ya asilimia 15, mwelekeo huu wa jumla unaficha tofauti za kikanda.

Ni wazi kwamba, Afrika Mashariki na Kusini zinatofautiana katika viwango vyao vya juu zaidi vya biashara ya ndani ya kanda, ambapo mauzo ya nje ya nchi za Afrika yanalingana na karibu 30% ya mauzo ya jumla ya kanda hizi. Maeneo haya yanatofautiana na sehemu nyingine za bara, ambapo biashara ina mwelekeo wa nje zaidi.

Eneo Huru la Biashara ya Bara la Afrika (AfCFTA) liliibuka kama mpango mkuu unaokusudiwa kushughulikia masuala haya ya biashara ya ndani ya Afrika. Lengo lake ni kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kuongeza mtiririko wa biashara ndani ya bara kwa kuunda soko moja la bidhaa na huduma.

Hata hivyo, licha ya uwezo wake, athari halisi ya AfCFTA imekuwa ndogo kufikia sasa, Ripoti hiyo ilisema.

Ripoti hiyo, imetolewa na UN DESA kwa ushirikiano na Tume tano za Kanda za Umoja wa Mataifa, UNCTAD, UN-OHRLLS na UNWTO, inaangazia mtazamo wa uchumi wa dunia wa 2024 na 2025, na utabiri wa ukuaji wa kikanda kwa chumi zilizoendelea na zinazoendelea, pamoja na chumi zilizo katika mpito.

Tipoti kamili inapatikana kuanzia tarehe 4 January 2024, saa 12:30 pm EST katika:Ìý