¹ú²úAV

UN nchini Mali: Tunauheshimu uamuzi wa serikali kuhusu kujiondoa kwa Ujumbe

Get monthly
e-newsletter

UN nchini Mali: Tunauheshimu uamuzi wa serikali kuhusu kujiondoa kwa Ujumbe

- El-Ghassim Wane, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali.
Franck Kuwonu
Afrika Upya: 
6 July 2023
UN Photo
El-Ghassim Wane, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu wa pande nyingi nchini Mali (MINUSMA), akitoa taarifa kwa mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Mali.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 
Sauti iko kwa Kiingereza.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita liliidhinisha kwa kauli moja kuondolewa kikamilifu kwa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Mali katika kipindi cha miezi sita ijayo. Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN na Mkuu wa Ujumbe wa Kimataifa wa Uimarishaji Nchini Mali (MINUSMA) Bw. El-Ghassim Wane alizungumza na Franck Kuwonu wa Afrika Upya kuhusu mafanikio, changamoto na mafunzo waliyojifunza. Kuna madondoo hapa:

Kwa wale ambao hawakufuatilia majadiliano ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (Security Council) tarehe 30 Juni 2023, unaweza kutoa muhtasari wa kile ulichoambia Baraza kuhusu hali nchini Mali?

Ilikuwa ni taarifa muhimu kwa sababu ilisadifiana na mjadala kuhusu kusasishwa kwa mamlaka ya Kimataifa ya Uimarishaji Nchini Mali (. Na kama unavyojua, muda wa mamlaka uliisha mnamo Juni 30. Kwa hivyo, niliichukua fursa hiyo kuripoti kuhusu maendeleo ya hivi karibuni katika robo ya mwaka. Haya kimsingi yanahusu suala la mpito nchini Mali na usaidizi tunaotoa kwa mchakato wa uchaguzi - wa vifaa, kiufundi, kifedha, lakini pia kisiasa.

Pia nilizungumza kuhusu mchakato wa amani (peace process), ambao umekuwa sehemu muhimu ya kipaumbele cha kimkakati cha ujumbe wetu. Mchakato huu kwa bahati mbaya umezuiwa tangu Disemba mwaka jana [2022] wakati washirika waliotia saini waliamua kusitisha ushiriki wao katika utaratibu wa ufuatiliaji wa makubaliano.

Aidha, nilizungumza kuhusu kazi tunayofanya katika sekta ya haki za binadamu, katika suala la kujenga uwezo kwa jeshi la Mali pamoja na uchunguzi tunaofanya kuhusu madai ya ukiukaji wa haki za binadamu. Ìý

Na kwa kumalizia, nilichukua fursa hiyo kuangazia kile ninachoamini ni mchango mkubwa wa kiutendaji na unaoonekana wa MINUSMA, kwa juhudi za kuleta utulivu wa Mali, huku nikionyesha kwamba inawezekana kufanya vyema zaidi na kwamba ni lazima tufanye vyema zaidi, lakini hili linaashiria ushirikiano wa karibu zaidi kwa upande wa utawala wa Mali.

Je, ni sahihi, kutokana na taarifa zinazotoka katika jiji kuu la Mali Bamako na kwenye ripoti yako, kusema kwamba hali ni tete kwa Mali na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa?

Bila shaka. Ninadhani tuko katika wakati muhimu kwa Ujumbe huo kwa sababu ni lazima uzingatie mustakabali wake katika muktadha wa uhusiano mbaya na taifa mwenyeji. Pia ni muktadha muhimu kwa Mali, ambayo iko katika hatua muhimu kwa mustakabali wake. Na kama unavyojua, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Mali alielezea ombi la taifa lake la kujiondoa kwa MINUSMA bila kuchelewa.

Wanajeshi wa MINUSMA wakilinda soko la kila wiki la Méneka.
MINUSMA

Katika mazingira haya magumu, Ujumbe huo bado unaweza kufanya nini?

Tuna jukumu kutoka kwa Baraza la Usalama la UN ambalo linaakisi mitazamo ya pande nyingi ya Umoja wa Mataifa kwa Mali na migogoro mingine mingi duniani kote. Mali inakabiliwa na hali ngumu sana katika suala la usalama wa taifa na hata mgogoro ambao kimsingi ni wa kisiasa. Kazi yetu ni kusaidia Mali kurejesha njia za kuhakikisha usalama wa ardhi yake na wa watu wake.

Kama sehemu ya jukumu hili, Ujumbe huo unafanya mengi, na umefanya mengi, katika kuunga mkono mchakato wa kisiasa. Ninadhani tumekuwa na jukumu muhimu katika kuunga mkono mpito, hasa mchakato wa uchaguzi, tukitoa mchango muhimu sana wa vipengele vingi vya kiufundi, kifedha na wa kiutaratibu.

Pia tunatekeleza jukumu muhimu katika upatanishi na uwezeshaji, tukishirikiana na Aljeria kama mpatanishi mkuu wa kimataifa kujaribu kuleta maoni ya wahusika karibu ili kufikia makubaliano.

Kuhusu utekelezaji wa makubaliano, tunatoa usaidizi wa kihalisia ili kuwezesha utiifu wa usitishaji mapigano kati ya pande zinazozozana. Kama Mwenyekiti wa Tume ya Kiufundi na Usalama, ambayo ina jukumu mahususi la kuhakikisha utiifu wa usitishaji mapigano, tunatoa usaidizi mkubwa katika suala la kulinda raia katika maeneo ambayo tumetumwa.

Ni wazi kwamba ulinzi wa kimwili hauwezekani kila mahali lakini kazi tunayoifanya inatambuliwa na kuthaminiwa na raia kwa sababu wanaweza kuona athari yake.

Katibu Mkuu wa UN António Guterres ameyafanya yafuatayo:
  • Ameipongeza operesheni ya kudumisha usalama na wafanyakazi wake.
  • Ametoa wito wa ushirikiano kamili wa Serikali ya mpito kwa manufaa ya kujiondooa kwa njia taratibu na salama kwa wafanyikazi na mali ya Ujumbe huo katika miezi ijayo.
  • Amezitaka pande zote zilizotia saini Mkataba waÌý2015 wa Amani na Maridhiano nchini Mali (2015 Agreement on ¹ú²úAV and Reconciliation in Mali)Ìýkuendelea kuheshimu usitishaji mapigano huku MINUSMA ikijiondoa.
  • Ana wasiwasi na hali kwamba kiwango na muda wa mamlaka yaÌýahadi ya kifedhaÌýinayohitajika ili kuwezesha mchakato wa kukopa umepunguzwaÌýmno wakati wa majadiliaano ya bajeti katikaÌýKamati ya Tano (Fifth Committee) ya Baraza kuu. ÌýHali hii inaongeza ugumu na na hatari za mchakato wa ukopaji.
  • Ataendelea kushirikiana na Serikali ya mpito kuhusu namna bora ya kuhudumia maslahi ya watu wa Mali kwa ushirikiano na Timu ya Umoja wa Mataifa nchini Mali, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Afrika Magharibi na Sahel (UNOWAS) na washirika wengine.

Pia tunafanya kazi muhimu, hasa kupitia upatanisho kati ya jamii, kuunga mkono upanuzi wa mamlaka ya serikali, na tunatekeleza makumi, kama sio mamia ya miradi ya kusaidia raia katika maeneo ambapo serikali haipo au ambapo uwepo wake ni mdogo.

Usaidizi wa aina hii pia unazijumuisha taasisi za serikali ya Mali, ili kuzisaidia kuimarisha uwezo wao.

Kisha, bila shaka, tuna jukumu la kuwezesha usaidizi wa kibinadamu, kukuza na kulinda haki za binadamu kwa kujenga uwezo wa taasisi husika za Mali, ikiwa ni pamoja na Vikosi vya Ulinzi na Usalama, lakini ambayo pia kuishia katika uchunguzi wa madai ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Kazi hiyo ni nyeti kwa sababu si mara zote ambapo ripoti zetu zinapokelewa vyema na utawala wa Mali. Tunakumbana na vikwazo kwa uhuru wetu wa kutembea, uwezo wetu wa kufanya uchunguzi na hata wakati mwingine uwezo wa kuyatembelea maeneo yetu ya ya utendakazi kwa njia huru. Lakini ni jukumu letu na ni lazima litekelezwe.

Ni mafunzo gani tunayoweza kujifunza kutokana na athari zake tangu Ujumbe wenu ulipofika nyanjani?

Ninadhani athari imekuwa ya pande nyingi. Tuna unyenyekevu wa kutambua kwamba hali nchini Mali bado ni ngumu sana. Jukumu la Ujumbe huo ni kusindikiza na kuunga mkono juhudi za utawala wa Mali na wadau wengine wa Mali. Ujumbe huo pekee hauwezi kubadilisha hali nchini Mali.

Serikali ya Mali na mamlaka za kitaifa zina jukumu la kimsingi la kubadilisha hali nchini mwao, na tunayaunga mkono matumaini yao.

Ikiwa hali nchini Mali imezorota, si kosa la Ujumbe huo wala si la jamii ya kimataifa. Nadhani ni muhimu kulizingatia hilo.

Binafsi, ninaona mchango wa Ujumbe huo kwa njia kadhaa:

  • Kuna msaada muhimu ambao tunatoa kwa maelfu ya raia ambao, mara nyingi sana, wanaweza tu kuutegemea Ujumbe wetu kwa mambo fulani. Ninadhani hicho ni kipengele muhimu, na watu wanaonufaika na usaidizi huu bila shaka wanasema ni muhimu sana kwa sababu unaonekana.
  • Kuna kazi yote ambayo tumefanya kuwalinda raia katika maeneo ambayo tupo au hatupo. Katika idadi fulani ya maeneo, sisi ndio pekee tuliopo, na kwa mengine ambapo tupo na vikosi vya Ulinzi na Usalama, tunajaribu kuifanya kazi hii kwa pamoja. Nadhani hiki ni kipengele muhimu sana cha kazi tunayoifanya.
  • Pia kuna usaidizi wote tulionao kwa ajili ya uendeshaji mzuri wa kipindi cha mpito, na utekelezaji wa makubaliano ya amani. Hivi pia ni vipengele muhimu sana vya kazi yetu. Kazi yetu ya usaidizi inaendelea, bila kujali ugumu mkuu tunaoukabili.

Kupitia kuripoti kwetu, tumetekeleza jukumu muhimu sana katika kuweka suala la kulinda na kukuza haki za binadamu kuwa juu katika ajenda ya umma.

Ninadhani huu ni mchango muhimu huku tukitambua kuwa hali nchini Mali inasalia kuwa ngumu sana, na kwa hakika si nzuri kama ambavyo tungetaka.

Bila shaka, sisi tungeweza kufanya vyemai zaidi. Lakini kama nilivyosema, jukumu la jamii ya kimataifa ni kuunga mkono Mali, na si kuchukua nafasi ya utawala wake, na uwezo wetu wa kutenda kazi nyanjani na kuwa na ufanisi pia unategemea kiwango cha ushirikiano tunaopokea kutoka kwa utwala wa Mali.

MINUSMA itakapoondoka kama ilivyoombwa na utawala wa Mali, je, hiyo haitakuwa hasara kwa taifa hilo na raia?

Nitauwachia utawala wa Mali kutathmini hilo. Ninadhani kwamba, katika kuufanya uamuzi huu, wameangalia athari zote.

Ninachokijua kwa hakika, na tunachoweza kuthibitisha, ni kwamba Ujumbe huo umekuwa na athari zinazoonekana nchini Mali. Hakuna shaka juu yake.

Hata hivyo, huu ni uamuzi uliochukuliwa na Mali kama taifa huru, ambao ni wazi kwamba tutalazimika kuuheshimu.

Tumeweza kutathmini kwamba kwa raia, hii itakuwa hasara kubwa. Lakini tena, ni uamuzi uliochukuliwa na utawala wa Mali.

Ninaamini tumefanya, na tunaendelea kuleta athari. Sio kamilifu, la hasha, na tungefanya vyema zaidi ikiwa tungepewa ushirikiano bora.

Wanajeshi wa MINUSMA wakilinda soko la kila wiki la Méneka.
MINUSMA