AV

Jinsi uchukuzi wa malori kutumia mtindo wa Uber unavyobadilisha kabisa biashara barani Afrika

Get monthly
e-newsletter

Jinsi uchukuzi wa malori kutumia mtindo wa Uber unavyobadilisha kabisa biashara barani Afrika

Malori yaliyosajiliwa na madereva wameunganishwa mtandaoni, na kusawazishwa na mahitaji ya uchukuzi wa mizigo
Franck Kuwonu
Afrika Upya: 
7 July 2021
Malori yakipita katika bara la Afrika.
Africa Renewal/Franck Kuwonu
Idadi iliyoongezeka ya malori yanapita katika bara zima lakini mara kwa mara hukwama kwa siku nyingi kwenye mipaka ya kimataifa.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 
Sauti ya Kiingereza

Karim Dembele, dereva wa lori kutoka Mali, anatoka kwa lori lake alimokuwa akilala kidogo. Yuko Lomé, mji mkuu wa Togo akisubiri kuvuka mpaka kuingia nchi jirani ya Ghana, na kisha kusafiri kwa lori kwa umbali wa kilomita 720 hadi anakoenda, Abidjan, huko Cote d'Ivoire.

Kama vile madereva wengi wanaosubiri pande zote za barabara hii katika eneo la Kodjoviakope, lori lake halina mzigo baada ya kusafirisha rundo la karatasi za saruji (zinazotumiwa kutengeneza mifuko ya saruji) kwa kiwanda kinachofanya kazi katika eneo la viwanda kilomita 10 huko Lomé.

"Nimekuwa nikingoja kwa siku mbili sasa, lakini inaweza kuchukua wiki hadi nitakaposikia kutoka kwa mkubwa wangu kuwa ni wakati wa kuendelea na safari," Bwana Dembele anaiambia Afrika Upya.

Katika siku hii yenye joto kali mwezi wa Mei, ikiwa imeathiriwa kidogo na upepo kutoka Bahari ya Atlantiki, barabara hii haina magari wala shughuli nyingi na maeneo ya karibu yametulia mno. Wachuuzi hawachuuzi bidhaa zao kama hapo awali na baa karibu na ufuo ziko tupu. Kwa sababu ya vikwazo vya COVID-19 wakati huo, wapita njia na aina tofauti za usafiri hazikuruhusiwa kuvuka na hivyo kulikuwa na utulivu fulani katika eneo hilo.

Kama vile lori la Bwana Dembele, malori mengi hayana mizigo na yameegeshwa bila kazi kwa siku kadhaa. Ni machache tu yaliyo na bidhaa. Malori mengine yanaelekea Bandari ya Tema, mengine Accra kisha Abidjan kupeleka au kuchukua bidhaa.

Huku idadi kubwa ya malori ikipitia bara lote, idadi yao kubwa, pindi tu yanapofikisha bidhaa hizo, hurudi bila mizigo.

Kwamba mengi ya malori haya yalikuwa yameegeshwa hapa bila kazi na kwamba madereva hawakuwa na habari au udhibiti wa harakati zao za safari inayofuata inaonyesha changamoto za uchukuzi ambazo malori yanakumbana nazo katika nchi nyingi barani.

Mtandao bora ulioratibiwa unaweza kuleta ufanisi zaidi, kupunguza muda wa kusafiri na kushusha gharama za mizigo.

Barani, biashara zilizoanzishwa hivi karibuni kama Lori Systems ya Kenya, Kobo360 nchini Nijeria, na nyingine kadhaa, zinajitokeza kuziba pengo hilo, kwa msaada wa wawekezaji wa kimataifa.

Kobo360, iliyozinduliwa mwaka wa 2018 nchini Nijeria, inajitambulisha kama kampuni ya teknolojia inayolenga kufikia ufanisi - "kampuni ambayo inakusanya shughuli mwanzo hadi mwisho kusaidia wamiliki wa mizigo, wamiliki wa malori, madereva na wapokeaji wa mizigo kuwa na mfumo bora wa usambazaji'' kulingana na tovuti yake.

Kulingana na mwanzilishi mwenza wake, Obi Ozor, kampuni ilianza wakati, kama mwanafunzi wa vyuo vikuu nchini Marekani, aligundua jinsi usafirishaji wa mizigo barabarani ulivyochukua muda mwingi katika nchi yake Nijeria ulivyoongeza gharama kubwa kwa kuingiza nepi, na kufanya bidhaa muhimu kama hii kuwa ya bei ghali kwa wengi

Ugumu wa uchukuzi unaongeza malipo ya 40-60% kwa gharama ya bidhaa, kote barani, kulingana na ripoti ya pamoja ya Google na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC), iliyotolewa Novemba iliyopita.

Katika Afrika Mashariki, malengo ya Lori Systems ya Kenya sio tofauti. Ilianzishwa mwaka wa 2016 na kuanza kutumika mwaka wa 2019, kampuni hiyo inakusudia "kuunganisha wamiliki wa mizigo kwa uchukuzi" ili "kupunguza gharama za bidhaa barani Afrika".

"Tunavyotumia malori hayasafiri mbali bila mizigo, ambayo inaweza kuwa gharama kubwa, tunaamini kwamba bei zitaendelea kushuka," Jean-Claude Homawoo, mwanzilishi mwenza wa Lori Systems, aliiambia CNN Business Disemba iliyopita .

"Tunasimamia mifumo ya makumi ya maelfu ya malori," alielezea, "na tuna uwezo wa kuyafanya yapatikane yanapohitajika."

"We manage a network of tens of thousands of trucks," he explained, “and are able to make them available as needed.”

Huku soko la uchukuzi na uhifadhi la bara likikadiriwa kufikia bilioni 80 za Marekani katika miaka miwili ijayo, kampuni kama hizo zinavuruga mifano ya zamani ya biashara ya malori kwa kutumia zana za kidijitali ili kulinganisha mahitaji na upatikanaji, na mahitaji na maagizo kwa njia bora zaidi.

Lori linaloharibika ghafla "sio tatizo," na pia mizigo fulani isipokuwa tayari. Lori lingine linaweza kutumwa kwa urahisi lingine likiharibika au kutumwa kwingine mizigo isipokuwa tayari kusafirishwa, alisema Bwana Homawoo.

Kampuni hiyo inafanya kazi Afrika Mashariki, huku mtandao kuu wa Kobo360 ukitumiwa Afrika Magharibi.

Ufanisi

Huku soko la uchukuzi na uhifadhi la bara likikadiriwa kufikia bilioni 80 za Marekani katika miaka miwili ijayo, kampuni kama hizo zinavuruga mifumo ya zamani ya biashara ya malori kwa kutumia zana za kidijitali ili kuunganisha mahitaji na upatikanaji, na mahitaji na maagizo kwa njia bora zaidi.

Biashara hizo zimeundwa kwa njia kama ya Uber ambapo wamiliki wa lori na madereva waliosajiliwa wameunganishwa kabisa na kulinganishwa na mahitaji.

Mnamo mwaka wa 2019, Kobo360 ilitajwa kuwa 'Mvurugaji wa Mwaka' na jukwaa la Wakurugenzi Watendaji wa Afrika, kwa kutambua athari yake ya haraka kwa safari ndefu huko Afrika Magharibi.

Hata hivyo, kama mfano huo wa uvurugaji ulivyo, makampuni ya uchukuzi ya kiubunifu ndipo yamenza tu. Yanahitaji kukua na kuwa endelevu kwa muda mrefu. Ili hili lifanyike, kiwango kikubwa cha hela kinahitajika. Wawekezaji wa kimataifa wamekuwa wakionyesha nia.

Kwa pamoja, Kobo360, Lori Systems, na Sendy (pia yenye makao yake Kenya), na yamekusanya angalau dola milioni 65 kutoka IFC na wawekezaji wengine katika miaka miwili iliyopita.

Biashara zinazoanzishwa za E-logistics ni muhimu katika kukuza uchumi wa mtandao wa Afrika, ambayo inaweza kuwa na thamani ya dola bilioni 180 kati ya 2023 na 2025, kulingana na ripoti ya Google-IFC. Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza, uwekazaji katika muundomsingi bado unasalia kupungukiwa kwa dola bilioni 67 hadi bilioni 107 kila mwaka.

Kwa hivyo maslahi ya wawekezaji wa kimataifa na ahadi za kuongeza shughuli zikijumuishwa pamoja, kampuni hizi zinafanya kazi chini ya theluthi moja ya nchi za Kiafrika. Na sio malori yote yanajua ahadi hizi.

Bwana Dembele, dereva wa lori kutoka Mali, haonekani kujua sana kuhusu njia mpya za malori. Wakati alitarajia kubeba bidhaa zingine huku akienda kuchukua mzigo mpya wa rundo la karatasi za saruji akirudi Togo, anategemea mawasiliano ya mdomo kutoka kwa wauzaji wengine wa lori kwenye njia yake ili kupata fursa.

Kujisajili kwa huduma mojawapo ya biashara hizi zinazoanzishwa kunaweza kurahisisha safari yake. Ingawa, hata ikiwa angetaka, hajui jinsi atakavyonufaika yeye mwenyewe, alisema.

''Mini ni dereva tu. Popote ambapo mmiliki ananiambia niende, kawaida huwa naenda. Yeye ndiye anayejua mizigo iko wapi na ananiambia nichukue wapi au nipeleke wapi, ”alisema.

Kwa kweli, soko bado halijafikiwa na ahadi za kuongezeka kwa biashara chini ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) zinaweza kuwa msukumo ambao sekta hii inahitaji ili kupanuka.