¹ú²úAV

Vijana wanaweza kuongoza Afrika siku za usoni

Get monthly
e-newsletter

Vijana wanaweza kuongoza Afrika siku za usoni

— Aya Chebbi
Raphael Obonyo
9 April 2019
Aya Chebbi, African Union Youth Envoy
Aya Chebbi, Balozi wa Vijana wa Umoja wa Mataifa

Unatarajia kutimiza mambo yapi katika muda wako wa kuhudumu?

Nina wajubu wa kutetea utekelezaji wa Mkataba wa Vijana wa Afrika, Ruwaza ya Mapato ya Makundi na Ajenda 2063. Naliona jukumu langu kama mjenzi wa daraja, kujenga uaminifu kwa kuziba mwanya wa habari kati ya Umoja wa Afrika na vijana wa Afrika, ambao unaweza kufikiwa kwa mkakati jasiri na imara wa mawasiliano na kwa kubuni nafasi muhumu jumuishi za mazungumzo kwa vijana katika Kamisheni ya Umoja wa Afrika. Aidha, ninafaa kuendeleza mazungumzo kuhusu muungano kuanzia ngazi ya jamii, kushughulikia pengo kati ya wazee na vijana wa Afrika. Pia nina mpango wa kusaidia kuhamasisha vijana kuhusu Uafrika, kuwaleta karibu na ruwaza yetu ya Uafrika, ambayo ni kuongoza katika juhudi za kufikia matarajio ya Ajenda 2063.

Tunaweza kufikia haya kwa ushirikiano, usaidizi, kushiriki na uratibu wa vijana wenyewe. Huu ni mchakato wa "kufanyakazi pamoja"—kusikiliza, kugawana, kutenda na kuinua sauti za vijana.

Ni mambo yapi unayoyapa kipaumbele?

Nitasema, kwanza ni nguzo nne za Ruwaza ya Mapato ya Makundi Afrika: uchumi, elimu, afya na utawala (hususani kwa vijana wanawake). Pia nitalenga masuala yanayowakumba wakimbizi, wanaorundi makwao na wahamaji wa kimataifa. Kama unavyojua, kauli mbiu ya Umoja wa Afrika ya 2019 ni "Wakimbizi, wanaorundi makwao na wahamaji wa kimataifa."

Kati ya wale wasiokuwa na ajira barani Afrika, vijana ni asilimia 60. Je,Ìý tunawezaje kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa vijana? Ìý

Tunahitaji kuanzisha haraka mazungumzo na mataifa wanachama kuhusu hali ya ajira barani Afrika. Licha ya kwamba kuna jitihada ya kushughulikia kuongezwa kwa nafasi za kazi, tunaonekana kuongeza nafasi zinazotoweka baada ya miaka michache. Kuna umuhimu wa kuwa na mazungumzo haya pamoja na matendo ya dharura ya kuongeza nafasi za ajira kwa vijana. Ningependa kuona Kamisheni ya Umoja wa Afrika ikianzisha Hazina ya Umoja wa Afrika ya Maendeleo ya Vijana ili kusaidia miradi ya biashara inayoanzishwa na vijana.ÌýÌý Kuanzishwa kwa Hazina ya maendeleo ya vijana katika ngazi za kanda na kitaifa inaweza pia kusaidia kuongeza nafasi za ajira kwa vijana. Aidha, ni muhimu kusaidia vijana kwa kuwapa mafuzo ya kazi, mipango ya kitaaluma, mafundisho na tajriba chanya.

Mkataba wa Vijana wa Afrika wa 2006, ni mfumo wa kuleta pamoja jitihada za kuwawezesha vijana kuimarisha maendeleo barani. Je,Ìý utelekezaji wake unaendeleaje?ÌýÌý

Kwanza, ni lazima tuhakikishe kuwa nchi zote zimeratibu na kukubali mkataba huu. Kuhusu na utekelezaji, bado kuna mengi ya kufanya katika maeneo mengi, kama vile kutoa ajira, maisha endelevu, elimu, afya, ushiriki wa vijana na kadhalika.

Je, vijana wanawezaje kushiriki kikamilifu na kufaidika kutokana na maeneo huru ya kufanyia biashara barani Afrika (AfCFTA)?

Kama sehemu ya mradi wa ushirikiano wa kiuchumi, AfCFTAÌý ni hatua moja kuelekea mbele. Kuunda nafasi za kazi kupitia biashara ya kitaifa kunaweza kuwavunja moyo vijana na kuwafanya kuhama nje ya Afrika kutafuta nafasi bora. AfCFTA inahitaji mataifa ya Afrika kuongezea bidhaa zao thamani na kuimarisha sekta yao ya huduma. Ili vijana wafaidike kwa soko kubwa la Afrika, mataifa lazima yarekebishe mitaala ya elimu kuhakikisha kuwa maarifa na ujuzi zinatolewa kwa mahitaji ya soko. Vijana sharti wabuni uwezo wa ujasiriamali. Kuna haja ya kuimarisha sayansi, teknolojia, uhandisi, hisabati na ujasiriamali katika shule.Ìý Vijana wana nafasi bora ya kushiriki katika uchumi wa kidijitali.

Je, mpango wako wa kuwahamasisha vijana kuhusu Umoja wa Afrika na Kamisheni yake ni upi?

Umoja wa Afrika ni asasi iliyoundwa kwa msingi wa thamani ya Uafrika na hatufai kupoteza matumanini kwake. Muungano huu una urithi wa uhuru wetu na maisha yetu ya pamoja. Aidha,Ìý ni muhimu kufahamu jinsi Umoja wa Afrika ulivyopangwa ili kuweza kudhibiti matarajio yetu na yale tunayoweza kufikia. Umoja wa Afrika kama asasi ya kikanda hauna mamlaka ya kupitisha au kutekeleza sera katika mataifa binafsi. Hii inabakia kuwa changamoto kuu katika kutekeleza mifumo ya sera na mada zilizopitishwa na Mkutano wa Umoja wa Afrika.Ìý Tunafaa kuimarisha na kubadilisha Kamisheni ya Umoja wa Afrika ili iweze kuwa na ufanisi zaidi. Vijana wanafaa kuhimizwa kuongoza baadhi ya taasisi zake. Nilikubali uteuzi huu kwa sababu nina imani kuwa Umoja wa Afrika utabakia kuwa nguzo muhimu ya umoja wetu.

Afrika Upya: Je, ilikuwaje hadi ukateuliwa kuwa balozi wa vijana wa Umoja wa Afrika?

Bi. Chebbi: Niliteuliwa kupitia mchakato ulio wazi. Kulikuwa na nafasi iliyotangazwa mtandaoni kwa vijana kutuma maombi. Nilituma maombi na nikawa mmoja kati ya watu 706 waliotuma maombi. Kati yao, 17 waliingizwa katika orodha fupi. Baada ya hapo, watu 4, nikiwepo, walialikwa kuhojiwa.Ìý Jopo la watu 14 walituhoji. Lilikuwa jopo kubwa kuwahi kunihoji. Kila mwanajopo alifaa kutuza alama kulingana na masharti yaliyowekwa. Nilikuwa na jumla ya alama za juu zaidi ya wote. Ìý

Je,Ìý nini ujumbe wako wa mwisho kwa vijana wa Afrika?

Ujumbe wangu ni kuwa,Ìý unaweza kuwa chochote utakacho maishani. Kuna mambo mawili tu unayofaa kufanya: banisha utambulisho wako na uishi kwa kuongozwa na lengo lako. Unahitaji kujifahamu mwenyewe na kujua unachokithamini. Ukishafahamu utambulisho wako, tambua ni kwa nini unaamka kila siku na unalolifanya kila siku, hilo ndilo lengo lako. Nataka uteuzi wangu uwe msukumo kwa vijana wa Afrika kutafuta nafasi za uongozi popote walipo katika chochote wanachokifanya. Ningetaka kuongeza kwamba vijana wanafaa kuwaÌý na hamu ya kuwa na Uafrika. Tumekuwa tukizungumzia sana miaka ya sitini na harakati za uhuru zilizotuongoza. Sasa tunafaa kuwa na uafrika wa karne ya 21, ili kuongoza bara hili kuelekea lipasavyo kuelekea. Siku zijazo za Afrika ziko imara tukiungana katika ruwaza ya pamoja ya uafrika kuwa, uhuru wangu ni wako pia.

Ìý

Ìý

Ìý

Ìý

Ìý