AV

Mshikamano, matumaini na ushirikiano vyahitajika kukabili COVID-19 -Guterres

Get monthly
e-newsletter

Mshikamano, matumaini na ushirikiano vyahitajika kukabili COVID-19 -Guterres

UN News
20 March 2020
By: 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akifanya mkutano kupitia mtandao kuhusu janga la kimataifa la COVID-19
UN Photo/Loey Felipe
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akifanya mkutano kupitia mtandao kuhusu janga la kimataifa la COVID-19

Wakati hofu ikiendelea kutanda kote duniani kufuatia kusambaa kwa mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema“sasa kuliko wakati mwingine wowote tunahitaji mshikamano, tumaini na utashi wa kisiasa ili kukabiliana na janga hili kwa pamoja.”

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao mjini New York Marekani hii leo Guterres amesema tofauti na majanga mengine makubwa ya kimataifa ya kiafya katika miaka 75 ya historia ya Umoja wa Mataifa “janga la virusi vya corona linasambaza madhila kwa binadamu na kuathiri uchumi wa dunia. Familia yetu ya kibinadamu inakabiliwa na shinikizo na ukuta wa kijamii umepasuka, watu wanateseka, wanaumwa na kuogopa.”

Ameongeza kuwa na kwa kuwa ngazi ya taifa haiwezi peke yake kukabiliana na changamoto hii ya kiwango cha kimataifa hivyo“sera za pamoja na bunifu zinahitajika kuanzia kwenye mataifa yanayoongoza kiuchumi duniani.”

Bwana. Guterres amesema kwamba anatarajia kushiriki mkutano wa dharura wa viongozi wa nchi tajiri 20 au G-20 utaofanyika wiki ijayo kwa lengo la kuchua hatua kukabiliana na changamoto ya janga hili.

Ukurasa kuhusu virusivyacorona & taarifa mpya
Wasomaji wanaweza kupata taarifa na muongozo kuhusu mlipuko wa virusi vya corona (2019-nCoV) kutoka Umoja wa Mataifa, Shirika la afya duniani na mashirika mengine ya UN hapa.
Kwa habari mpya kila siku kutoka UN News, bofya hapa.

“Ujumbe wangu mkuu uko bayana , tuko katika hali ngumu na sheria zetu za kawaida hazifanyi kazi tena. Tuko katika vita na virusi vya Corona hivyo mitazamo bunifu ni lazima iende sanjari na asili ya janga hili na hatua tunazochukua lazima ziendane na ukubwa wa janga hili.”

Katibu Mkuu ameongeza kuwa ingawa COVID-19 inaua wat una kuathiri uchumi kwa kuudhibiti vyema janga hili tunaweza kujijenga upya kuelekea katika njia ambayo ni endelevu na jumuishi.“Natoa wito kwa viongozi wote wa dunia kuja pamoja na kuchukua hatua za haraka na za pamoja kukabiliana na zahma hii ya kimataifa.”

Dharura ya afya

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kushughulikia dharuya ya kiafya ni kipaumbele chake cha kwanza na anachagiza juhudi zaidi na za bila ubaguzi za kusaidia katika upimaji, kuwasaidia wahudumu wa afya na kuhakikisha vifaa vya kutosha.

“Imethibitika kwamba virusi hivyo vinaweza kudhibitiwa , n ani lazima vidhibitiwe , ni wakati wa kuondokana na mkakati wa nchi mojamoja na kuhamia katika mkakati wa kimataifa kukabiliana na janga hili ikiwepo kuzisaidia nchi ambazo hazijajiandaa vyema kukabiliana na zahma hii.”

Ameongeza kuwa“Mshikamano wa kimataifa sio tu ni muhimu kidhamira , lakini pia ni suala lenye maslahi kwa kila mtu“ amesema na kuzitaka serikali kutimiza maombi yote yaakisema tunakuwa imara tu kwa pamoja wakati mifumo yetu ya afya ikiwa imezidiwa.

" Mshikamano wa kimataifa sio tu ni muhimu lakini pia ni suala la maslahi ya kila mtu-Mkuu wa UN "

Hatuna najuhudi za kujikwamu

Kama kipaumbele chache cha pili Bwana. Guterres ametaja athari za kijamii na kiuchumi na jisni ya kujikwamua . amegusia ripoti mpya ya shirika la kazi duniani () ikikadiria kwamba wafanyakazi wnaweza kupoteza dola trilioni 3.4 za mapato ifikapo mwisho wa mwaka.

Lakini amesema dunia haishuhudii mdororo mkubwa katika mnyororo wa usambazaji na mahitaji ni mshangao kwa jamii.

“La msingi zaidi tunapaswa kujikita na watu , wale wasiojiweza , wenye kipato kidogo, wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo. Hii inaamanisha kusaidia mshahara, bima, hifadhi ya jamii, kuzuia kufilisika na kupoteza ajira.”

Amefafanua kwamba “Kujikwamua kisije kwa mgogo wa masikini na hatuwezi kuunda kundi la masikini wapya hivyo ni lazima tuwasaidie walioko katika sekta zisizorasmi nan chi ambazo hazina uwezo wa kukabiliana na janga hili.”

Chonde chonde nyoosheni mkono

Akitoa ombi la msaada wa kifedha kimataifa ameainisha kwamba shirika la fedha duniani IMF, Benki ya Dunia na taasisi zingine za kimataifa za kifedha watakuwa na jukumu muhimu.

Guterres amechagiza kuondoa vikwazo vya kibiashara na kuanzisha upya mnyororo wa usambazaji. Pia ameelezea athari za zahma hii kwa wanawake akisema kwamba “wanabeba mzigo mkubwa nyumbani, katika uchumi na kwa watoto ambao amesema zaidi ya milioni 800 hawako madarasani hivi sasa na wengi wao wakitegemea shule kwa ajili ya kupata mlo. “

Katibu mkuu ameongeza kwamba wakati maisha ya watu yakiathiriwa, kutengwa na kupinduliwa chini juu ni lazima kuzuia janga hili lisigeuke zaiha ya afya ya akili. Kuna haja ya kuhakikisha program za msaada kwa wasiojiweza na mahitaji ya kibinadamu yasipuuzwe.

Kujikwamua vyema

Na suala la mwisho la Katibu mkuu ni kwamba tuna jukumu la kujikwamua vyema katika janga hili.“Ni lazima tuhakikishe kwamba tumejifunza na kwamba zahma hii inatupa fursa ya maandalizi ya mifumo ya afya na kwamba uwekezaji katika karne ya 21 kwenye huduma za umma ni muhimu .”

Akigusia ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 na mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris amesema “ni lazima tutimize ahadi yetu kwa wat una sayari dunia.”