AV

Chapisho la Africa Renewal la Umoja wa Mataifa lawapa heko wafanyakazi wa afya wa COVID-19 walioko katika mstari wa mbele Afrika

Get monthly
e-newsletter

Chapisho la Africa Renewal la Umoja wa Mataifa lawapa heko wafanyakazi wa afya wa COVID-19 walioko katika mstari wa mbele Afrika

Africa Renewal
15 May 2020

Wakati ulimwengu ulikaa kama umesimama kwa sababu ya COVID-19, wafanyakazi wa afya walikuwa katika mstari wa mbele kupambana na janga hili kushinda wengine wote maishani.

Barani Afrika, kama ilivyo katika sehemu nyingi ulimwenguni, madaktari, wauguzi, wakunga, wanafamasia, wataalamu wa matibabu, madaktari wa meno, madereva wa ambulensi, na wengine wengi wanajitolea kuokoa maisha ndani ya changamoto kadhaa. Kujitolea kwao mhanga kumeleta tofauti kubwa katika mapambano ya jumla ya janga hili.

Ni kwa sababu hii ambapo chapisho la Africa Renewal la Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika ̶ linaendesha kampeni mtandaoni kusherehekea wale mashujaa walio kwenye mstari wa mbele wa kupambana na COVID-19 barani Afrika. Tutachapisha masimulizi yao katika wavuti wetu na kwenye Facebook na Twitter.

Wakati tunathamini ujasiri wao, bidii na uvumilivu, tunasisitiza pia umuhimu wa kazi yao wakati wa janga hili.

NINI: Kampeni mtandaoni kusherehekea wafanyakazi wa afya barani Afrika.

NANI: Madakatari, wauguzi, wataalamu wa maabara, maofisa wa kimatibabu, wanaradiolojia, wakunga, wasaidizi wa kimatibabu, wataalamu wa matibabu, wanafamasia, madereva wa ambulensi, wanaojitolea, n a wengine kwenye kundi hili.

KWA NINI: Kuwafanya wafanyakazi wa afya kujua kuwa wanathaminiwa na kuwatia moyo katika kazi yao.

LINI: Kuanzia tarehe 18 Mei hadi Julai 2020

VIPI: Kwa kuangazia masimulizi yao katika mtandao wa Africa Renewal na kwenye Facebook na Twitter.

Unawezaje kushiriki? Kwa namna mbili: jaza fomu hii hapa chini au ututumie baruapepe

Je, wewe ni mfanyakazi wa afya wa anayepambana na COVID-19 katika mstari wa mbele barani Afrika? Tutumie masimulizi yako (kwa kujibu maswali yaliyo hapa chini) na picha kwenye anwani: africarenewal@un.org

1. Tufahamishe kidogo kukuhusu? (Jina, umri, jiji/mji, nchi, kazi, jina la eneo lako la kazi)

2. Je, umekuwa ukifanya kazi kama mhudumu wa afya kwa muda gani? Je, nini ilikufanya kuchagua kazi ya huduma ya afya? Uko na hofu au majuto yoyote?

3. Je, unasaidiaje kupambana na COVID-19 katika nchi yako? Je, kazi yako imebadilikaje tangu kulipuka kwa COVID-19?

4. Je, nini kinakuathiri sana katika janga hili la COVID-19? Je, nini kinakufanya kuzidi kuendelea na unaikabili hali vipi?

5. Kwa mtazamo wako, ni mkakati gani, uliofanya vyema katika mapambano haya na nini gani haukufaulu? Je, lipi linafaa kufanywa kushinda vita dhidi ya COVID-19?

6. Je, nini ujumbe wako kwa watu wa nchi yako, na kwa wengine barani Afrika wakati huu wa COVID-19?

Je, unajua mfanyakazi wa afya wa anayepambana na COVID-19 katika mstari wa mbele Afrika? Wateue kwa kutuma majibu ya maswali haya kwa: africarenewal@un.org

1. Jina lako, jiji na nchi.

2. Jina la mfanyakazi wa afya unayemteua?

3. Jina la jiji lake na nchi?

4. Jina la hospitali au kituo cha afya anakofanya kazi?

5. Jina la jiji na nchi?

6. Sababu za kumteua?

Mada: