AV

Janga la COVID-19 linazidisha dharura ya kuwa na njia nyingi za mapato ya kiuchumi barani Afrika

Get monthly
e-newsletter

Janga la COVID-19 linazidisha dharura ya kuwa na njia nyingi za mapato ya kiuchumi barani Afrika

Kufanya mambo kama kawaida katika kipindi cha baada ya janga kutazidisha matatizo ya kiuchumi
Njuguna Ndung’u
Afrika Upya: 
8 September 2020
Bandari huko Tema, Ghana.
Jonathan Ernst / World Bank
Bandari huko Tema, Ghana.

Idadi ndogo ya mbinu za kuunda mapato ya kiuchumi ndiyo sababu kuu inayosababisha udhaifu wa kiuchumi barani Afrika. Isitoshe, janga la COVID-19 limeongeza hatari kwa nchini zinazotegemea pakubwa njia moja ya maliasili kama mafuta.

Afrika imejaliwa maliasili nyingi, ikiwemo madini, na mapato kutoka kwa mauzo yake ndio njia kuu ya kuleta mapato kwa nchi nyingi.

Njuguna Ndung’u
Njuguna Ndung’u

Aljeria, Angola, Libya na Nijeria kwa pamoja huzalisha sehemu kubwa ya mafuta duniani; Afrika Kusini na nchi zingine kadhaa za Kiafrika ni eneo kuu la pato linatolokana na dhahabu ulimwenguni.

Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Sierra Leone ni nchi zenye wingi wa almasi. Madini mengine muhimu kama chrome, coltan, bauxite na manganese hupatikana katika nchi kadhaa za bara Afrika. Isitoshe, bara hili ni eneo muhimu kwa kuni gumu za kitropiki, kahawa, kakao na mpira.

Kutegemea shughuli moja ya kiuchumi au bidhaa chache za mauzo ya nje na uagizaji ni hatari kwa uchumi wa kitaifa. umeongea sana dhidi ya nchi za Afrika kutegemea pakubwa bidhaa za kuchimbwa ili ziweze kuwa na njia nyingi za kuunda mapato ya kiuchumi.

inatabiri kuwa kwa sababu ya janga la COVID-19, chumi za mataifa yaliyo kusini mwa jangwa la Sahara huenda zitapatwa na mfumuko wa kiuchumi kwa kuwa Pato la Taifa linatarajiwa kupungua kutoka asilimia 2.4 mwaka wa 2019 hadi kati ya asilimia -2.1 na asilimia -5.1 mwaka wa 2020.

Katika makala yenye mada ya Shanta Devarajan, mtaalamu wa zamani wa uchumi kutoka Benki ya Dunia, James Cust na Pierre Mandon, ambao pia ni wataalamu wa uchumi, wanasisitiza kuwa maliasili husababisha kuongezeka kwa matumizi ya serikali ambayo hatimaye husababisha athari hasi katika ushindani.

Nadharia ya Bwana Devarajan inafafanua ni kwa sababu gani laana ya maliasili imekuwa sugu kwa chumi za Afrika.

Makala yake—na makala mengine ya utafiti kuhusu mada hiyo—yalichapishwa na , taasisi ya utafiti na ujenzi wa uwezo.

Wafanyabiashara wanapakua magunia ya vitunguu katika soko la wakulima huko Bamako, Mali.
Dominic Chavez/World Bank

Lengo la AERC ni kuwafahamisha watunga sera barani Afrika kuhusu maarifa ya ulimwengu kuhusu namna ya kusimamia maliasili chini ya hali endelevu.

Afrika imepiga hatua ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika miongo miwili iliyopita, lakini kuwa na njia nyingi za mapato ya uchumi kungeweka msingi thabiti zaidi wa maendeleo ya haraka. Chumi ambazo hazina njia nyingi za mapato ya kiuchumi zilipata upungufu wa ukuaji, zikiambatana na taasisi dhaifu, pamoja na juhudi zilizodumaa katika mageuzi ya kimuundo na kiuchumi.

Chumi zilizodhoofishwa kwa ukosefu wa njia nyingi za mapato zinaweza kukabiliwa na dharura ya ulimwengu kama janga. Mifumo mibovu ya afya na ni masuala yanayotatiza maeneo yanayostawi.

, shirika la sera linalolenga maendeleo endelevu, ilisisitiza kwamba, “Mataifa ya Afrika ni miongoni mwa mataifa yaliyopatwa bila mipango yoyote [na janga hili], yenye mifumo dhaifu mno ya afya na yanayotegemea sana njia za kilimwengu za kuongeza thamani.”

IIED inaendelea kuonya kuwa kupungua kwa thamani ya sarafu kulikosababishwa na kuongezaka kwa upungufu wa sasa wa fedha kutaleta matatizo kwa nchi ambazo zinategemea sana uagizaji wa chakula na mafuta.

Kuwa na njia nyingi za mapato ya kiuchumi baada ya COVID-19

Kwa hivyo, nchi, haswa zile zilizo katika hatari zaidi, lazima zitekeleze sera na mikakati inayojikita kwenye ithibati na ambazo zinakuza njia nyingi za mapato ya kiuchumi.

Mojawapo ya mikakati kama hiyo ni ujumuishaji wa kifedha unaoendeshwa na mapinduzi ya kidijitali ili kukuza ujumuishaji wa soko na shughuli za uzalishaji kwa gharama ya chini zaidi. Majukwaa ya kidijitali pia yanaweza kukuza uzalishaji wa kilimo kupitia malipo ya haraka ya mazao, kubadilishana habari na shughuli za kilimo-viwanda.

Utafiti na uvumbuzi lazima uchukue jukumu muhimu katika kuongeza uhimilivu wa uchumi.

Mkakati mwingine ni kuondoa vikwazo kwa biashara barani Afrika na biashara na maeneo mengine. Vikwazo kwa biashara vinajumuisha sera tatizi za kuagiza na kuuza nje, ushuru wa biashara na michakato migumu ya forodha. Kwa bahati nzuri, utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) linatarajiwa kushughulikia vikwazo hivi.

Kiwango cha chini cha mseto wa uchumi wa Afrika ni sababu inayoongoza kwa udhaifu wa uchumi wa bara.

Isitoshe, kuongezeka kwa uzalishaji wa ndani, haswa na viwanda vya kilimo, kutashughulikia uvurugaji unaosababishwa na kutegemea sana uagizaji wa chakula kutoka nje ya bara. Kila nchi inaweza kuongeza faida na utaalamu wake wa kiulinganishi.

Ujenzi wa uwezo wa kitaasisi na kugeukia rasilimali safi ni hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa na nchi. Rasilimali safi zitasaidia matumizi ya malighafi inayotumika kuzalisha nishati kupitia viwanda vya gesi na umeme.

Mikakati hii inahitaji kuongeza uwekezaji na tija—kutoka sekta kibinafsi, ya umma, na uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni—katika maendeleo ya kiuchumi na miundombinu ambayo yatapunguza gharama za matumizi na kutoa nafasi kwa sekta binafsi kupata faida.

Inashauriwa kupitisha mtazamo bora katika utekelezaji wa vidhibiti vya kukabili mishtuko ya janga la siku zijazo.

Ni kweli kwamba nchi kadhaa za Kiafrika zimepitisha ruwaza ya kimkakati kuimarisha njia zao za maendeleo. Hata hivyo, nchi zingine zimeshindwa kutekeleza sera na mikakati mwafaka ya kufikia ruwaza zao, na hivyo kupoteza imani kutoka kwa raia na sekta binafsi.

Umuhimu wa kuwa na njia nyingi za mapato ya kiuchumi na mageuzi ya muundo wa kiuchumi ni swala lililo wazi. Kufanya biashara kama kawaida katika kipindi cha baada ya janga hili kunazidisha ugumu wa kiuchumi.

Swali muhimu ni jinsi nchi zinaweza kuunda na kutekeleza sera haraka kusaidia kupona haraka na pia kujikinga dhidi ya majanga ya siku zijazo. Historia imeonyesha kuwa ni rahisi kuanzisha mageuzi wakati wa janga kama hili la sasa. Afrika lazima sasa iamke.


ProfesaNjuguna Ndung’u ni Profesa Mwandamizi wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya, na alihudumu kama Gavana wa Benki Kuu ya Kenya kutoka Machi 2007 hadi Machi 2015.

Njuguna Ndung’u
More from this author