AV

Viongozi wa ulimwengu wahimizwa kuongeza usaidizi kwa pango wa the Great Blue Wall

Get monthly
e-newsletter

Viongozi wa ulimwengu wahimizwa kuongeza usaidizi kwa pango wa the Great Blue Wall

Ni juhudi inayoongozwa na Afrika inayolenga kuwezesha uwezo wa uchumi wa baharini na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika Kanda ya Bahari Hindi Magharibi
Afrika Upya: 
9 Novemba 2022
Na: 

Viongozi wa ulimwengu wanaohudhuria kongamano la mabadiliko ya tabianchi linalofanyika Sharm El Sheikh, Misri, wameonyesha shauku na kuahidi kuharakisha hatua kuhusu mpango wa Great Blue Wall.

Bahari ndizo karo kubwa zaidi la kupunguza joto duniani; inafyonza karibu 90% ya joto la ziada linalosababishwa na mabadiliko ya tabianchi na pia ni makaro ya kaboni yenye ufanisi sana, ikifyonza 23% ya kaboni inayotolewa na binadamu. Bahari ni mshirika wetu mkubwa katika mapambano ya hatua ya tabianchi, lakini, kwa bahati mbaya, tunahatarisha suluhisho hili kwa kutozilinda.
Dr. Mahmoud Mohieldin
UNFCCC Mabingwa wa Ngazi ya Juu wa Tabianchi wa Umoja wa Mataifa

Mpango wa "Great Blue Wall" (GBW) ni juhudi zinazoongozwa na Afrika kufikia ulimwengu wenye asili chanya ambao huongeza unyumbufu wa sayari na jamii kusitisha na kubatilisha upotevu wa asili ifikapo 2030.

Unalenga kuunda maeneo ya baharini yaliyounganishwa, yanayolindwa na yaliyohifadhiwa ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la joto duniani katika kanda ya Bahari Hindi Magharibi (WIO).

Unalenga pia kufungua uwezo wa uchumi wa baharini kuwa kichocheo cha uhifadhi wa asili na matokeo ya maendeleo endelevu.

"Sisi sote hapa ni watetezi, waendelezaji, na viongozi katika nafasi ya bahari. Tunapaswa kuikabili changamoto hii, na hatuwezi kufanya hili peke yetu; inabidi ziwe juhudi za pamoja,” alisema Rais Wavel Ramkalawan wa Ushelisheli.

Rais alisisitiza haja ya wote "kuacha kuzungumza kuhusu Bahari Hindi, Bahari ya Pasifiki, na Bahari ya Atlantiki," na badala yake "kuzungumza kuhusu bahari moja ambayo lazima tuilinde."

Alikuwa akizungumza katika hafla iliyoandaliwa kwa pamoja na UNECA, serikali ya Ushelisheli, Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN), na Mabingwa wa Ngazi ya Juu wa Tabianchi wa Umoja wa Mataifa.

Great Blue Wall ni mpango unaoongozwa na Waafrika ambao unadhihirisha maadili ya Umoja wa Afrika wa suluhu za Afrika kwa matatizo ya Afrika
Ms. Josefa Sacko
Kamishna wa Umoja wa Afrika wa Kilimo, Maendeleo ya Mashambanii, Uchumi wa baharini, na Mazingira Endelevu

Wazungumzaji wengine wa ngazi za juu walijumuisha Balozi Peter Thomson, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari; Nigel Topping; Bingwa wa Ngazi ya Juu ya Tabianchi wa UNFCCC, Børge Brende, Rais, Jukwaa la Uchumi Duniani na wawakilishi kutoka Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na maafisa kutoka serikali za Kenya na Msumbiji.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Rais wa IUCN, Razan al Mubarak, alisema mpango wa Great Blue Wall "umepata uungwaji mkono kutoka ndani na nje ya Afrika, na umeinua hadhi ya hali mbaya ya bahari yetu na kurejesha nguvu na imani katika ushirikiano wa kimataifa.

Mahmoud Mohieldin - Bingwa wa Ngazi ya Juu wa Tabianchi wa UNFCCC - alisisitiza umuhimu wa uhifadhi wa bahari, akibainisha, "bahari ni mshirika wetu mkubwa katika mapambano ya hatua ya tabianchi, lakini, kwa bahati mbaya, tunahatarisha suluhisho hili kwa kutozilinda."

“Bahari ndizo karo kubwa zaidi la kupunguza joto duniani; inafyonza karibu 90% ya joto la ziada linalosababishwa na mabadiliko ya tabianchi na pia ni makaro ya kaboni yenye ufanisi sana, ikifyonza 23% ya kaboni inayotolewa na binadamu," alisema Bw. Mohieldin.

Linahusu kupiga hatua kutoka kuonyesha kile kinachowezekana hadi kukwea kwa hatua nyingine ya kiwango na matarajio ili tuwe na mchanganyiko wa uhifadhi wa asili na uwezeshaji jamii za mitaa kuwa na vitekauchumii endelevu
Mr. Antonio Pedro
Kaimu Katibu Mtendaji wa UNECA

Tukio hilo, ambalo liliangazia uhusiano wa mabadiliko ya tabianchi, uhifadhi wa asili, na uchumi wa baharini, lilionyesha mpango wa kikanda wa kwanza wa aina yake unaoendeshwa na athari - GBW - kuongeza na kuharakisha hatua kuhusu tabianchi na bahari katika Afrika. Pia ilionyesha jinsi matukio muhimu ya kimataifa yanaweza kuwa hatua za kufikia malengo ya GBW; na kutoa wito kwa vyama na washirika kutoa msaada na ushirikiano.

Kamishna wa Umoja wa Afrika wa Kilimo, Maendeleo ya Mashambanii, Uchumi wa baharini, na Mazingira Endelevu, Josefa Sacko, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na ufumbuzi unaoongozwa na Afrika kwa matatizo ya Afrika.

"Ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako, ukitaka kwenda mbali, nenda na wenzako - lazima tufanye kazi bega kwa bega. Great Blue Wall ni mpango unaoongozwa na Waafrika ambao unadhihirisha maadili ya Umoja wa Afrika wa suluhu za Afrika kwa matatizo ya Afrika,” alisema Bi. Sacko.

Kuhusu hatua za mbeleni kwa mpango wa GBW, Nigel Topping, Bingwa wa Ngazi ya Juu ya Tabianchi wa UNFCCC, aliangazia hitaji la kuzingatia uhamasishaji wa ufadhili wa miradi ya tabianchi, kufanya kazi kikanda, na kuzingatia sayansi na nguvu ili kuwavutia wawekezaji.

Kaimu Katibu Mtendaji wa UNECA, Antonio Pedro, alisisitiza umuhimu wa utekelezaji.

"Linahusu kupiga hatua kutoka kuonyesha kile kinachowezekana hadi kukwea kwa hatua nyingine ya kiwango na matarajio ili tuwe na mchanganyiko wa uhifadhi wa asili na uwezeshaji jamii za mitaa kuwa na vitekauchumii endelevu," alisema Bw. Pedro.