AV

Walinda amani wanawake toka Brazil na India watwaa tuzo ya jinsia ya UN ya 2019

Get monthly
e-newsletter

Walinda amani wanawake toka Brazil na India watwaa tuzo ya jinsia ya UN ya 2019

UN News
27 May 2020
By: 
Washindi wa tuzo ya masuala ya jinsia ya Un mwaka 2020, Meja Suman Gawani (Kushoto) wa jeshi la India aliyetumika awali UNMISS na kamanda Carla Monteiro de Castro Araujo, afisa wa jeshi la anga la Brazil ambaye sasa anafanyakazi na MINUSCA
UNMISS/MINUSCA/Hervé Serefio
Washindi wa tuzo ya masuala ya jinsia ya Un mwaka 2020, Meja Suman Gawani (Kushoto) wa jeshi la India aliyetumika awali UNMISS na kamanda Carla Monteiro de Castro Araujo, afisa wa jeshi la anga la Brazil ambaye sasa anafanyakazi na MINUSCA

Mwanamke mlinda amani kutoka Brazil anayehudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na mlinda amani mwanamke kutoka India ambaye amehitimisha hivi karibuni jukumu lake nchini Sudan Kusini wamechaguliwa kupokea tuzo ya mwaka 2019 ya Umoja wa Mataifa ya mwanajeshi mchagizaji wa masuala ya kijinsia.

Washindi hao kamanda Carla Monteiro de Castro Araujo, afisa wa jeshi la anga la Brazili ambaye kwa sasa anahudumu kwenye mpango wa Umoja wa Matafa wa kurejesha utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Katina Meja Suman Gawani kutoka jeshi la India , mwanajeshi mwangalizi wa zamani wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, watapokea tuzo hiyo wakati wa hafla iyakaypfanyika mtandaoni ikiendeshwa kna Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kuadhiisha siku ya kimatafa ya walinda amani Ijumaa ya 29 Mei 2020.

Tuzo ya jinsia ya UN

Tuzo hiyo “Mwanajeshi mchagizaji wa mwaka wa masuala ya kijinsia”iliyoanzishwa mwaka 2016 inatambua kujitolea na juhudi za mwanajeshi mlinda amani katika kuchagiza misingi ya azilimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake, amani na ulasalma katika muktada wa operesheni za amni , wakipendekezwa na wakuu au makamanda wa operesheni za ulinzi wa amani.

Kwa mara ya kwanza wanawake wawili walindamani watapokea tuzo hiyo kwa Pamoja kwa mchango wao katika suala hili muhimu.

Baada ya kupokea taarifa za ushindi huo kamanda Monteoro de Castro Araujo amesema“Tuzo hii ni utambuzi wa kazi inayohusisha kikosi cha MINUSCA na kitengo cha raia. Ni jambo ya kurahisha na kuridhisha kwangu mimi na kwa mpango mzima kuona kwamba miradi yetu inazaa matunda.”

Naye Meja Gwani ameelezea faraja yake kwa kuona kazi yake kama askari mwangalizi wa Umoja wa Mataifa imetambuliwa“Kwa majukumu yetu yoyote, msimamo wetu au cheo chetu ni jukumu letu kama walinda amani kujumuisha mtazamo wa jinsia zote katika kazi yetu ya kila siku na kuumiliki. Katika muingiliano na wafanyakazi wenzetu, pamoja pia na jamii.”

Kamanda Monteiro

Kamanda Monteiro de Castro Araujo amehudumu kama mwanajeshi mshauri wa jinsia na ulinzi katika vikosi vya MINUSCA makao makuu tangu Aprili 2019.

Wakati wa muhula wake alianzisha na kuendesha mafunzo ya kina katika masuala yanayohusiana na jinsia na ulinzi.

Kupitia juhudi zake mpangoo huo uliongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya wasimamizi wa masuala ya jinsia na ulinzi na vituo pia.

Pia alikuwa chachu muhimu sana katika kushuhudia doria za hatua zinazohusisha masuala ya jinsia zikihusisha jamii zikiongezeka kutoka 574 hadi kufikia karibu 3000 kwa mwezi.

Meja Gawani

Tangu kupelekwa kwake UNMISS mwezi Desemba 2018 , Meja Gawani amewafundisha Zaidi ya waangalizi 230 wa jeshi la Umoja wa Mataifa (UNMO) kuhusu ukatili wa kingono unaohusiana na vita na kuhakikisha uwepo wa waangalizi wanajeshi wanawake katika kila timu ya vituo vya mpango huo.

Kwa kutoa msaada, ushauri, mwongozo na uongozi alisaidia kuunda mazingira ya kuwezesha walinda amani wa Umoja wa Mataifa

Pia alifundisha vikosi vya serikali ya Sudan Kusini na kuwasaidia kuzindua mpango mkakati wao wa kukabiliana na ukatili wa kingono uliohusiana na vita.

Hongera kwa kazi nzuri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza kamanda Monteiro de Castro Araujo na Meja Gawani kwa tuzo zao. “ Walinda amani haw ani mfano wa kuigwa. Kupitia kazi zao wameleta mitazamo mipya na wamesaidia kujenga Imani na ujasiri katika jamii tunazozitumikia.” Amesema Katibu Mkuu na kuongeza kwamba “kupitia kujitolea na njia zao za ubunifu wamekumbatia kiwango cha ubora ambacho ni msukumo mkubwa kwa walinda amani wote kila mahali. Tunapokabiliana na changamoto za sasa kazi yao haijawahi kufaa au kuwa na umuhimu zaidi kama wakati huu.”

Huu ni mwaka wa pili mfululizo mlinda amani kutoka Brazil anapokea tuzo huu ya heshima n ani mara ya kwanza tuzo hii kwenda kwa mlinda amani kutoka India.