AV

Mradi wa Kigoma wa FAO unaolenga wanafunzi ni ufunguo wa mazao bora

Get monthly
e-newsletter

Mradi wa Kigoma wa FAO unaolenga wanafunzi ni ufunguo wa mazao bora

UN News
18 October 2019
By: 
Wanafunzi kutoka shule ya msingi ya Minyinyi, nchini Tanzania na mwalimu wao ambaye anawafundisha kutumia kifaa cha kupima rutuba kwenye ardhi kwa ajili ya vipimo vya mbolea.
FAO Tanzania
Wanafunzi kutoka shule ya msingi ya Minyinyi, nchini Tanzania na mwalimu wao ambaye anawafundisha kutumia kifaa cha kupima rutuba kwenye ardhi kwa ajili ya vipimo vya mbolea.

Kutokomeza umasikini uliokithiri ni kitovu cha juhudi za dunia kufikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na kujenga mustakabali endelevu kwa watu wote lakini mafanikio ya kutomwacha yeyote nyuma hayatapatikana iwapo watu walioachwa nyuma zaidi hawatalengwa kwanza.

Hiyo ni sehemu ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres katika kuadhimisha siku ya kutokomeza umasikini duniani hii leo Oktoba 17.

Mwaka huu kaulimbiu imejikita katika“kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kuwawezesha watoto, familia zao na jamii kwa ajili ya kutokomeza umasikini wakati tukiadhimisha miaka 30 tangu kuasisiwa kwa mkataba wa haki za mtoto."

Umoja wa Mataifa umesema watoto wako katika hatari maradufu zaidi ya kuishi katika umasikini uliokithiri kuliko watu wazima huku umasikini ukiwaweka watoto katika hali ngumu ya ukosefu na kuzua hatari ya kupitisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Kwa kutambua umuhimu wa kuwawezesha watoto, shirika la kilimo na chakula duniani,nchini Tanzania kupitia mradi wa programu ya pamoja ya Kigoma nchini humo wanaendesha mradi wa kuwawezesha wanafunzi kupima ardhi ili kutambua kiwango cha rutuba na hivyo kuweka mbolea inayofaa kwa ajili ya kupata mazao bora, huyu ni mmoja wa wanafunzi mnufaika wa mradi kutoka shule ya Minyinyi iliyoko wilaya ya Kigoma Kaskazini magharibi mwa Tanzania

(Sauti ya mwanafunzi)

Mwalimu Rochas Katabizi ni mwalimu katika shule hiyo ya Minyinyi

(Sauti ya mwalimu)

Umoja wa Mataifa umesema lengo moja la kutokomeza umasikini ni kukabiliana nao katika kaya ambako kwa kawaida unaanzia.

Mada: