AV

Miji yenye mfumo bora wa elimu, ni mfano wa kuigwa-UNESCO

Get monthly
e-newsletter

Miji yenye mfumo bora wa elimu, ni mfano wa kuigwa-UNESCO

UN News
28 January 2020
By: 
Jiji la Tianjin China
World Bank/Yang Aijun
Jiji la Tianjin China

Mtandao wa miji iliyotambuliwa na UNESCO kuwa miji yenye mfumo bora wa elimu, GNLC ni mifano michache ya kufanya ujifunzaji kuwa sehemu ya msingi ya jamii ambazo haziachi nyuma mtu yeyote. Mtandao huo unaunga mkono harakati za kusongesha malengo yote ya maendeleo endelevu hususani lengo na 4 linalosisitiza elibu bora kwa wote na la 11 la miji bora endelevu. Miongoni mwa miji hiyo ni Gdynia ulioko nchini Poland.

Bartosz Bartoszewicz ni Naibu Meya wa mji huo anayesimamia maisha bora, anasema,“elimu ni, na mara zote imekuwa kipaumbele cha juu cha Gdynia. Ni moja ya vitu ambavyo vinatengeneza maisha bora katika Gdynia, moja ya miji bora nchini. Shule za Gdynia zinawaruhusu wakazi wetu wa umri wa chini kuendeleza matamanio na vipaji vyao. Hayani matunda ya kuhusishwa kwa watu kadhaa. Kwa upande mmoja walimu, wakuu wa shule, watoa huduma na maafisa wa utawala. Lakini kwa upande mwingine pia ni matokeo ya uchapakazi wa wanafunzi na ushiriki wa wazazi wao. Hii ni shukrani kamili kwa ushirikiano huu kwamba elimu ya Gdynia iko tayari kwa changamoto mpya, katika kuibadilisha dunia na wote tunaweza kufanya kazi pamoja kuufanya mfumo huu kuwa bora iwezekanavyo.”

Mji huo wa Gdynia si tu unashughulika na elimu ya watoto bali pia unawasaidia watu wazima kuelimika.

Mji mwingine ilioko katika mtandao wa miji inayotambuliwa nakuwa miji yenye mifumo bora ya elimu ni Groningen, huko nchini Uholanzi. Carine Bloemhoff ni naibu Meya anaeleza wanachofanya akisema,“katika manispaa yetu, tunatakiwa kukiri kwamba, katika familia unamokulia, ndiyo inaamua fursa utakazopata katika maisha. Wakati huo huo tunaona ongezeko la mgawanyiko wa shule katika manispaa yetu. Wazazi wenye elimu kidogo wanawapeleka watoto wao katika shule fulani, na wazazi wenye elimu ya juu wanafanya hivyo kwa kuwapeleka watoto wao katika shule nyingine. Matokeo yake, watoto hawa hawatakuja kukutana. Na tunataka kulibadilisha hilo. Kwa pamoja na wataalamu wa elimu.Tunataka kupambana na kutengana huku. Kwa pamoja na wadau wetu katika elimu tunachunguza vikwazo vyote, kuanzia shule za awali za kulea watoto hadi sekondari na kwa namna gani tunaweza kujifunza kutoka kwao ili kulenga fursa sawa. Watoto wa wazazi wanaofanya kazi wanaenda katika shule za kulea watoto wadogo wakati watoto wa wazazi wasiofanya kazi wanabaki nyumbani. Hapa ndipo utengano katika jamii unapoanzia. Tumechukua hatua kuhakikisha kila mtoto anaweza kwenda katika shule ya awali angalau saa 16 kwa wiki. Nje ya hapo tumeanzisha mtu ambaye tunamwita afisa wa upatanishi ambaye ni kama daraja kati ya shule na nyumbani. Mtoto aliyeko katika hali ngumu aanakutana na kila aina ya matatizo. Afisa huyu wa upatanishi ataweza kusaidia. Kwa mifano kwa kumtambua mtoto fulani anaweza kutumia mfuko wa michezo ya vijana au akaomba wakfu wa Leergeld kununua vifaa vya shule. Elimu bora ni muhimu kwa mstakabali wa watoto wote mjini Groningen. Ndiyo maana tunataka kushiriki.”