AV

Mchango wa Balozi Mahiga hautosahaulika -Balozi Manongi

Get monthly
e-newsletter

Mchango wa Balozi Mahiga hautosahaulika -Balozi Manongi

UN News
5 May 2020
By: 
Augustine Mahiga, (katikati) Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN nchini Somalia akizungumza na wanajeshi kutoka ujumbe wa Muungano wa Afrika Somalia, AMISOM, kwenye makao makuu Mogadishu, 24 Januari 2012.
AU-UN IST PHOTO / STUART PRICE
Augustine Mahiga, (katikati) Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN nchini Somalia akizungumza na wanajeshi kutoka ujumbe wa Muungano wa Afrika Somalia, AMISOM, kwenye makao makuu Mogadishu, 24 Januari 2012.

Kwa watu waliofanyakazi kwa karibu na Balozi Mahiga wakati wa uhai wakewanasema alikuwa mfano wa mfano wa kuigwa na wanajivunia sana kumfahamu.

Miongoni mwa watu hao waliowahi kufanyakazi na mwendazake Balozi Mahiga ni aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Tuvako Manongi, ambaye anasema asilani mchango wake hautosagaulika si tu kwa Tanzania hata kwenye Umoja wa Mataifa lakini pia katika Idhaa ya Kiswahili ya Umoja huo.

Ni kweli Balozi Mahiga atakumbukwa na watu wengi.Haswa wale tuliobahatika kufanya kazi chini yake ama pamoja naye katika Umoja wa Mataifa tutamkumbuka kwa mambo makubwa.Labda sita ama saba hivi kwanza inaeleweka kwamba kwa upande wa kukuza lugha ya Kiswahili katika Umoja wa Mataifa Mahiga alijitahidi sana kuimarisha kitengo cha idara ya kiswahili hasa kuhakikisha kwamba kimepata bajeti stahili na ambayo inajitegemea. Pili alihimiza sana kupanuliwa na kuongezwa kwa watangazaji kutoka nchi zinazo ongea lugha ya kiswahili.

Balozi Mahiga pia ameacha alama isiyofutika katika masuala ya amani ya Umoja wa Mataifa

Tatu ni kweli balozi Mahiga alisimamia sana kupanuliwa na kuongezeka kwa ushiriki la jeshi la wananchi wa Tanzania yaani TPDF katika vikosi vya ulinzi vya Umoja wa Mataifa. Nne itakumbukwa kwamba balozi Mahiga alikuwa mwenye kiti mwenza katika kuunda chombo muhimu sana cha Umoja wa Mataifa cha kukuza amani katika nchi zenye migogoro chombo nikacho itwa peacebuilding commision.Chombo hiki kilianzishwa mwaka 2015 kama chombo maalum cha kuishauri baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu migogoro mahali popote pale duniani na balozi Mahiga ndiye aliyekuwa mwenyekiti mwenza katika kuanzisha chombo hicho.Tano,ni muhimu kukumbuka kuwa bwana Mahiga alikuwa chachu sana katika kubadilisha dhana ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa inatawala k wakati huo kutoka kwa vikosi vya kusimamia utekelezaji wa amani hadi vikosi vinavyoweza kupambana na kudhibiti vikosi vya wasio wanao vunja amani kilikuwa ni kitu kikubwa sana ambacho mwishoni kilisababisha kuvunjwa au kupigwa kwa kile kikundi cha M23 nchini DRC.

Na katika Umoja wa Mataifa hakuwa balozi tu alishika pia nyadhifa mbalimbali

La sita ni kwamba balozi Mahiga alitumikia Umoja wa Mataifa kama mwakilishi wa nchi washirika la wakimbizi kule India alishiriki kuwa mfanyakazi wa shirika la wakimbizi lilo kule makao makuu ya Umoja wa Mataifa kule GenevaUswisi. Pili vilevile balozi Mahiga alikuwa mwakilishi maalum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia mwaka wa 2010 .Mwisho Balozi Mahiga amewakilisha Tanzania kwa uaminifu na uadhilifu mkubwa sana,mara baada ya taarifa za kifo chake balozi Ombeni Sefue ambaye ndiye aliyechukua nafasi ya balozi Mahiga pale Umoja wa Mataifa alitutaarifu kundi la mabalozi ambao wamewahi kutumikia nchi zao katika Umoja wa Mataifa habari hii ya msiba huu salamu za rambirambi zimetoka pahala pote duniani kutoka filipino,Uingereza, Marekani, Amerika ya Kusini visiwa vya Carribean,India,Sri Lanka,Bangladeshi na kote duniani. Mabalozi wote walikuwa wanaeleza na mkusifia balozi Mahiga kama mtu ambaye alikuwa Mchapa kazi na mtu aliyekuwa na unyenyekevu na umahiri mkubwa sana. Hivyo balozi Mahiga amefariki lakini kifo ni uamuzi na mapenzi ya mwenyezimungu.Lakini pamoja na kifo hicho familia ya balozi Mahiga, na wale ambao tumefanya kazi nao wanakila sababu ya kujivunia sana maisha yake na utendaji wake kwa taifa letu na jumuia ya Mataifa .Huyo ndio balozi Mahiga ninaye mfahamu na balozi ambaye kwa kweli tunakila sababu ya kujivunia hayo maisha na jitihada zake.Ni mtu wa kuigwa na watu wote.

Ama kwa hakika Balozi Mahiga mwendo umeumaliza , pumzika kwa amani.