AV

Makundi yaliyojihamini marufuku kuingiza watoto jeshini: Fally Ipupa

Get monthly
e-newsletter

Makundi yaliyojihamini marufuku kuingiza watoto jeshini: Fally Ipupa

UN News
By: 
Askari watoto nchini DRC.Umoja wa Mataifa wataka mataifa yote kuafiki kutowatumia watoto katika migogoro ya kijeshi. Picha: UN Photo/Marie Frechon
Picha: UN Photo/Marie Frechon. Askari watoto nchini DRC.Umoja wa Mataifa wataka mataifa yote kuafiki kutowatumia watoto katika migogoro ya kijeshi.
Picha: UN Photo/Marie Frechon. Askari watoto nchini DRC.Umoja wa Mataifa wataka mataifa yote kuafiki kutowatumia watoto katika migogoro ya kijeshi.

Makundi mbalimbali yaliyojihami kwa silaha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, yameaswa kuwajibika na kuhakikisha hayawaingizi watoto jeshini, kuwapa vyeo na kuwashirikisha vitani.

Wito huo umetolewa na balozi mwema wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini DRC wa MUNUSCO , katika vita dhidi ya kutumikisha watoto vitani ambaye ni mwanamuziki nyota Fally Ipupa.

Akizungumza baada ya kuzuru kituo cha muda cha watoto waliookolewa kutoka kwenye makundi ya wapiganaji (CAJED) mjini Goma ambako alipata fursa ya kuzungumza na watoto hao kupata hali halisi Ipupa amesema

(SAUTI YA FALLY PUPA)

Nafikiri kwamba si vizuri kutumikisha watoto. Inapaswa watoto wasalie kwenye familia zao, ili waende shuleni, waishi maisha ya kawaida. Inatakiwa iwapo mzazi akiona mtoto wake wa kike au wa kiume amebeba silaha ili kwenda kwenye mapigano, nadhani si vema, kwa kuwa nilipozungumza na mhusika wa MONUSCO hapa Goma, alinieleza kuwa wapo kwenye mchakato wa mashauriano na wale wanaotumikisha watoto ili hatimaye watoto waweze kufikia ndoto zao.

Kwa mujibu wa MONUSCO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, Ipupa ambaye almeteuliwa wiki hii kuwa balozi mwema wa MONUSCO mchango wake kupitia sauti yake utasaidi sana katika kuelimisha umma wakiwemo mashabiki wake kuhusu tatizo la utumikishaji wa watoto jeshini.