AV

Kuhusu haki za wanawake huu sio wakati wa kuridhika -Bachelet

Get monthly
e-newsletter

Kuhusu haki za wanawake huu sio wakati wa kuridhika -Bachelet

UN News
27 February 2020
By: 
Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.
UN Photo/ Jean-Marc Ferré
Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Tunapaswa daima kusherehekea mafanikio ya Beijing, lakini lazima tukumbuke kwamba mpango huu wa kuchukua hatua haujakamilika amesema leo kamishna mkuu wa haki za binadamu Michelle Bachelet mjini Geneva.

Bi Bachelet ameyasema hayo kwenye Baraza la haki za binadamu wakati wa jopo la majadiliano ya kuadhimisha miaka 25 ya jukwaa la Beijing la kuchukua hatua kwa ajili ya kuwawezesha wanawake azimio lililopitishwa mwaka 1995 akisisitiza kwamba“hakuna muda wa kurudhika na kubweteka”.

Kwa mujibu wa Bi.Bachelet hatari ya kupiga hatua nyuma ipo bayana na inaongezeka , amesema kama mkutano wa Beijing unatambukika ni wakati wa ahadi na maamuzi ya pamoja kuhusu haki za binadamu , miaka 25 baadaye mazingita ni tofauti kabisa. Kwa mantiki hiyo amesema kwamba “Haki za wanawake zinashambuliwa na ziko katika tishio kubwa katika nyanja nyingi”

Utu wa binadamu haiwezi kutengwa, kugawanywa, kujadiliwa, au kuwa fursa ya wachache - Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu.

Ameongeza kuwa “tunashukudia kudorora kwa hatua na kuibuka kwa hadithi za pengo la usawa wa kijinsia kwa misingi ya ubaguzi wa kizamani .”

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa “haki za binadamu za wanawake si suala la mjadala, haziwezi kuwa ni chaguo la sera linaloendanda na mwelekeo wa mabadiliko ya kisiasa”.

Amesisitiza kwamba hatuwezi na hatutotaka kuisambaratisha agenda ya haki za wanawake kwa kuanzisha ngazi baina ya hatua zinazokubalika na zile zinaozoonekana ni nyeti.

Kwa lugha nyingine ni kuiialika jumuiya ya kimataifa kukabiliana na changamoto kubwa za ubaguzi na kukubali ukweli kwamba “haki za wanawake ni haki za binadamu kwa dunia na kwa kila mtu, kwa ajili ya wanawake wote kikamilifu na kwa uhuru. Amehimiza kwamba utu wa binadamu hauwezi kutengwa, kugawanywa, kujadiliwa au kuwa fursa ya walio wachache.

UN Women yadhamiria kuchagiza vijana na dini

Kwa mujibu wa Bi. Bachelet“Makubaliano ya kihistoria ya Beijing si ya bahati wala si ajali ni matokeo ya hatua za makusud zilizochukuliwa na serikali, asas iza kiraia na wadau wengine.”

Katika miaka 25 iliyopita amesema tumefanikiwa kutekeleza masuala kafdhaa mazuri na tuna nyenzo za kuendeleza mchakato zaidi huku tukiwataka wadau mbalimbali kusaka mshikamano na maono pia. Kuliko madhumuni na dhamira ya Beijing.

Hivi ndivyo anavyoichukulia dunia inayopiga hatua kuelekea jamii zenye usawa na jumuishi , lakini pia jamii ambazo zimejizatiti kutomuacha yeyote nyuma.

Mchakato usio sawia

Phumzile Mlambo-Ngucka, Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women akizungumza na wanahabari kuhusu ripoti ya Usawa wa jinsia katika utekelezaji ajenda 2030
Phumzile Mlambo-Ngucka, Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women akizungumza na wanahabari kuhusu ripoti ya Usawa wa jinsia katika utekelezaji ajenda 2030
UN /Eskinder Debebe

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women Phumzile Mlango-Ngcuka amesema“mchakato unakwenda taratibu na haulingani ukijumuisha pengo kubwa katika soko la ajira.”

Ameongeza kuwa ingawa kiwango cha ajira kimepungua katika miaka ya karibuni , wanawake wengi wameajiriwa na wanafanya kazi zanyumbani zisizo na malipo. Pia ukatili dhidi ya wanawake na wasichana unaendelea na kusalia kuwa ni mgogoro wa kimataifa.

Amesema katika hali hii hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa nan chi wanachama ni lazima zitekeleze ahadi ilizozitoa kwenye jukwaa la kimataifa la Beijing la kuchukua hatua.

Na UN Women inajitahidi kuwachagiza wadau ambao hawakuwepo Beijing kama vile vijana na mdini ili kupata mawazo mapya na rasilimali.