AV

Guterres aelezea kusikitishwa na madhara ya kimbunga Idai, WFP yajizatiti kuwasilisha misaada

Get monthly
e-newsletter

Guterres aelezea kusikitishwa na madhara ya kimbunga Idai, WFP yajizatiti kuwasilisha misaada

UN News
By: 
Une vue aérienne au dessus d'une région du Mozambique touchée par les inondations causées par le cyclone tropical Idai
UN Mozambique
Umoja wa Mataifa Msumbiji tayari unawasaidia walioathirika na mafuriko yaliyotokana na kimbunga IDAI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea kusikitishwa kwake na vifo, uharibifu wa mali na kufurushwa kwa watu kufuatia mvua kubwa na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Idai.

Bwana Antonio Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake ametoa salamu za rambirambi kwa familia na waathirika na kwa watu na serikali ya Zimbabwe.

Halikadhalika taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imemnukuu akielezeamshikamano waUmoja wa Mataifa na mamlaka Zimbabwe na kuelezea utayari wa Umoja huo kufanya kazi nao wakati huu wakijibu mahitaji ya kibinadamu yanayotokana na jangah ilo.

Wakati huo huo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP limewasilisha tani 20 za msaada wa chakula wa dharura mwishoni mwa juma hili kwa njia ya ndege.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa WFP Herve Verhoosel, shirika hilo pia kwa ushirikiano na serikali zimetoa boti 30 kwa ajili ya kusafirisha chakula nchini Msumbiji kufuatia Kimbunga IDAI kuukumba mji wa bandari wa Beira nchini humo.

Kufuatia kimbunga hicho ambacho kimesababisha mafuriko makubwa ambayo yameshaathiri maeneo mengine Kusini mwa Afrika ikiwemo Kusini mwa Malawi na Mashariki mwa Zimbabwe, WFP limepeleka wafanyakazi Beira, Zambezi na Tete.

Bwana Verhoosel amesema WFP imewaslisha msaada wa kwanza kwa watu 6,000 walioathirika na mafuriko Tere kupitia mgao wa pesa taslimu kwa ushirikiano na wafanya biashara mashinani.

Aidha WFP imefadhili ndege zisizo na rubani kwa ajili ya ramana ya wakati wa dharura na zinatarajiwa kuwasilishwa Beira haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kusaidia tathmini ya mashirika. Pia WFP imekodisha helikopta kwa ajili ya operesheni za anga kwa ajili ya kufikia maeneo ambayo hayafikiki yaliyozingirwa na maji.

WFP katika kipindi cha siku chache zijazo itaimarisha mgao wa chakula ambapo kwa sasa makadirio yanaonyesha kwamba watu milioni 1.7 walikuwa katika hatari ya kukumbwa na kimbunga na watu 920,000 waliathirika Ma ,aelfu ziaid huko nchini Zimbabwe ambako tathmini inaendelea.

Nchini Malawi, WFP inatarajia kufikia watu 650,000 na msaada wa chakula nako Msumbiji ikilenga watu 600,000 kufuatia kimbunga IDAI.

Mada: