AV

COVID-19: Kijana Tanzania atengeneza ndoo ya kunawa mikono bila kugusa koki wala sabuni

Get monthly
e-newsletter

COVID-19: Kijana Tanzania atengeneza ndoo ya kunawa mikono bila kugusa koki wala sabuni

UN News
30 March 2020
By: 
Kijana Tanzania atengeneza ndoo ya kunawa mikono bila kugusa koki wala sabuni.
UN News/ UNIC Tanzania
Kijana Tanzania atengeneza ndoo ya kunawa mikono bila kugusa koki wala sabuni.

Ugonjwa wa virusi vya Corona, auCOVID-19ukiwa umeshasambaa katika mataifa 199 ikiwemo Tanzania, vijana nao wanaibuka na ubunifu mbalimbali ili kusaidia mataifa yao katika kudhibiti kuenea kwa gonjwa hilo lisilo na tiba wala chanjo. Ubunifu wa vifaa vya kudhibiti kuenea umefanywa na kijana mmoja nchini Tanzania kama anavyoripoti… wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam.

Jijini Dar es salaam nchini Tanzania katika moja ya karakana za uchomeleaji vyuma nakutana na kijana Joseph Sanga, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mbunifu wa ndoo ya kunawa mikono kwa maji na sabuni bila kushika koki wala sabuni.“Kwanza kabisa mashine hii, mfano wa kwanza nilifanya mwaka jana. Kwa maana ya kwamba nilijikita katika kuhakikisha kuwa tunanawa mikono bila kushika koki kwa sababu ya maambukizi ya magonjwa ya kuhara. Kwa hiyo niliangalia kwanza magonjwa ya kuhara, lakini baada ya kuja kwa gonjwa hili jipya baya nikaboresha ule mfano wa kwanza nikapta mashine hii ambayo yenyewe kwa kwasasa unanawa mikono kwa kukanyanga pedali na kisha unapata sabuni kwa kukanyaga pedali.

Pamoja na kusema kuwa kifaa hicho hakihitaij umeme na kinamudu mazingira magumu, Joseph akafafanua kinavyofanya kazi.“Hii ina pedali mbili, pedali ya kwanza ni kwa ajili ya sabuni na pedali ya pili ni kwa ajili ya maji.Lakini kwenye pedali hii ya maji, kadri unavyoisukumu ndivyo kadiri unavyoongeza kiwango cha maji kutoka.”

Gharama kwa ndoo moja na sabuni na ndoo ya kukingia maji machafu ni shilingi 150,000 za Tanzania sawa na takribani dola 70 za kimarekani,ambapo Joseph anasema faida ni ndogo sana hivyo ana ombi,«Nikipata fursa ya kuonana na Waziri nitamuomba angalau anisaidie kwenye hili ili niweze kusambaza hivi vifaa kwa bei ya chini ,nipate malighafi bila usumbufu, kodi pia niangaliwe ili nipate namna nzuri ili nisambaze vifaa zaidi na watu wengi zaidi wapate kunawa mikono.»