¹ú²úAV

Kila unachohitaji kujua kuhusu uchafuzi unaosababishwa na plastiki

Get monthly
e-newsletter

Kila unachohitaji kujua kuhusu uchafuzi unaosababishwa na plastiki

Afrika Upya: 
5 June 2023
Na: 
UNEP/Ahmed Nayim Yussuf
Ufungaji wa Sanaa ya Plastiki na Saype.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 
Sauti iko kwa Kiingereza.

Mwaka huu,Ìý inaangazia janga la uchafuzi unaosababishwa na plastiki. Sababu ni zipi? Binadamu wanazalisha zaidi yaÌýÌýza plastiki kila mwaka, thuluthi mbili kati ya hizo ni bidhaa za muda mfupi ambazoÌýhuharibika haraka, kujaza bahari na, mara nyingi, kuingia kwenye mfumo wa chakula cha binadamu. Hapa kuna maelezo yetu kuhusu janga la uchafuzi unaosababishwa na plastiki.

Swali: Je, kwa nini uchafuzi unaosababishwa na plastiki ni tatizo?

Jibu: Plastiki ya bei nafuu, ya kudumu, na badilifu, imeenea katika maisha ya kisasa, na kupatikana katika kila kitu kutoka kwa ufungaji, nguo na hata kwa bidhaa za urembo. Lakini plastiki hizi hutupwa kwa kiwango kikubwa: kila mwaka, zaidi ya tani milioni 280 za bidhaa za muda mfupi za plastiki huwa taka.

Kwa jumla,Ìý, huku asilimia 22 husimamiwa vibaya na husalia kama taka. Tofauti na vifaa vingine, plastiki haiozi. Plastiki inaweza kuchukua hadi , kwa hivyo zinapotupwa, zinajilimbikiza katika mazingira hadi kufikia hatua ya kuwa janga. Uchafuzi huu unatatiza wanyamapori wa baharini, huharibu udongo na kutia sumu kwenye maji ya ardhini, na unaweza.

Je, uchafuzi wa mazingira ndio tatizo pekee la plastiki?

La, pia inachangia mabadiliko ya tabianchi. Utengenezaji wa plastiki ni mojawapo ya michakato inayotumia nishati nyingi zaidi ulimwenguni. Bidha hii imetengenezwa kutoka kwa mafuta ya kisukuku kama vile mafuta ambayo bado hayajasafishwa, yanayobadilishwa kupitia joto na viungio vingine kuwa plastiki. Mnamo 2019, 3.4 ya jumla katika ngazi ya kimataifa.

Kuhusu Siku ya Mazingira Duniani
  • tarehe 5 Juni ndiyo siku kubwa zaidi ya kimataifa kwa mazingira.
  • Likiongozwa na UNEP na kufanyika kila mwaka tangu 1974, tukio hili limekua na kuwa jukwaa kubwa zaidi la kimataifa la kuhamasisha watu kuhusu mazingira, huku mamilioni ya watu kutoka kote ulimwenguni wakishiriki kuilinda sayari.
  • Mwaka huu, Siku ya Mazingira Duniani italenga suluhisho la janga la uchafuzi unaosababishwa na plastiki.

Je,Ìý plastiki hizi zote zinatoka wapi?

Sekta ya upakiaji ndiyo inayochangia zaidi taka za plastiki zinazotumika mara moja tu duniani.ÌýTakriban asilimia 36 ya plastiki zote zinazozalishwa hutumika katika vipakiaji. Asilimia hiyo inajumuisha vyombo vya plastiki vinavyotumika mara moja vya vyakula na vinywaji, asilimia 85 yake huishia kujaza ardhi au kama taka zisizodhibitiwa vizuri.

Ìýni eneo lingine ambalo plastiki ziko kila mahali: zinatumika katika kila kitu kutoka kwa kupaka mbegu na kufunika mchanga. Sekta ya uvuvi ni chanzo kingine kikubwa.Ìý unadokeza kuwa zaidi ya pauni milioni 100 za plastiki huingia baharini kutoka kwa zana za uvuvi za kiviwanda pekee.ÌýSekta ya mitindo ni mtumizi mwingine mkuu wa plastiki. Karibu asilimiaÌý, ikijumuisha poliyesta, akriliki na nailoni.

Nimesikia watu wakizungumza kuhusu plastiki ndogondogo. Je,Ìý hizo ni nini?

Ni vipande vidogo vya plastiki vinavyofikia urefu wa milimita 5. Zinatoka kwa kila kitu kutoka kwa magurudumu ya magari na bidhaa za urembo, ambazo zina miduara, chembe ndogo zinazotumika kama viondoaji. Chanzo kingine kikubwa ni vitambaa. Kila wakati nguo zinapofuliwa, vipande hivyo humwaga nyuzi ndogo za plastiki zinazoitwa vitamba vidogovidogo - aina ya vitambaa vidogo sana. Ufuaji pekee husababisha takriban tani 500,000 za nyuzi ndogo za plastiki kumwagwa baharini kila mwaka – sawa na karibu mashati bilioni 3 ya poliyesta.

Je,Ìý kunafanywa nini kuhusu uchafuzi unaosababishwa na plastiki?

Mnamo 2022, Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa zilikubaliana juu ya azimio la kukomesha uchafuzi unaosababishwa na plastiki. inaunda sheria kuhusu uchafuzi unaosababishwa na plastiki, na inalenga kuikamilisha ifikapo mwisho wa 2024. Muhimu ni kwamba, mazungumzo hayo yamelenga hatua zinazozingatia mzunguko mzima wa hali ya plastiki, kutoka uchimbaji na muundo wa bidhaa hadi uzalishaji na udhibiti wa taka, kuwezesha fursa za kuunda taka kabla hazijatengenezwa kama sehemu ya uchumi unaostawi.

Je, ni nini kingine kinachohitajika kufanywa?

Ingawa hatua hizi ni habari njema, ahadi za sasa za serikali na sekta hii hazitoshi. Ili kupambana kamili na janga la uchafuzi unaosababishwa na plastiki, mageuzi ya kimfumo yanahitajika. Hii ina maanisha, kuachana na uchumi wa sasa wa plastiki, unaozingatia kuzalisha, kutumia na kutupa plastiki, na kudumisha uchumi mzunguko ambapo plastiki inayozalishwa inahifadhiwa katika uchumi kwa thamani yake ya juu kwa muda mrefu iwezekanavyo.

Je, nchi zinawezaje kutekeleza haya?

Nchi zinahitaji kuhimiza uvumbuzi na kutoa ruzuku kwa biashara zinazoacha kutumia plastiki zisizo za lazima. Ushuru unahitajika ili kuzuia uzalishaji au matumizi ya bidhaa za plastiki zinazotumika mara moja, huku mapumziko ya ushuru, ruzuku na vivutio vingine vya kifedha vinahitaji kuanzishwa ili kuhimiza njia mbadala, kama vile bidhaa zinazoweza kutumika tena. Miundombinu ya udhibiti wa taka lazima pia iboreshwe. Serikali pia zinaweza kushiriki katika mchakato wa Kamati ya Majadiliano ya Kiserikali ili kuunda sheria za kushughulikia uchafuzi unaosababishwa na plastiki, ikijumuisha mazingira ya baharini.

Je, mtu wa kawaida anaweza kufanya nini kuhusu uchafuzi unaosababishwa na plastiki?

Huku janga la uchafuzi unaosababishwa na plastiki likihitaji mageuzi ya kimfumo, chaguzi za mtu binafsi huleta mabadiliko. Kama vile kubadilisha tabia ili kuepuka matumizi ya bidhaa za plastiki kila inapowezekana. Ikiwa bidhaa za plastiki haziwezi kuepukika, zinapaswa kutumika tena na tena hadi zisiweze kutumika tena - wakati huo zinapaswa kurejeshwa au kutupwa ipasavyo. Beba mifuko ukienda kwenye duka la mboga, na ikiwezekana, ujitahidi kununua vyakula vya asili na vya msimu ambavyo vinahitaji upakiaji na usafiri wa plastiki kwa kiwango kidogo.

Je, nishawishi serikali na biashara kushughulikia uchafuzi unaosababishwa na plastiki?

Ndio. Mojawapo ya hatua muhimu zaidi ambazo watu binafsi wanaweza kuchukua ni kuhakikisha sauti yao inasikika kwa kuzungumza na wawakilishi wao wa ndani kuhusu umuhimu wa suala hili na kusaidia biashara ambazo zinajitahidi kupunguza matumizi ya bidhaa za plastiki katika mifumo yao ya usambazaji. Watu binafsi wanaweza pia kuonyesha uungaji mkono kwenye mitandao ya kijamii. Watu wakiona kampuni ikitumia plastiki isiyo ya lazima (kama vile plastiki za matumizi ya mara moja zikifunika matunda kwenye duka la mboga) unaweza kuwasiliana nao na kuwahimiza kutofanya hivyo.

Mada: 
More from this author