AV

Namibia imekuwa nchi ya kwanza Kusini mwa Afrika kujiunga na Mkataba wa Maji wa Umoja wa Mataifa

Get monthly
e-newsletter

Namibia imekuwa nchi ya kwanza Kusini mwa Afrika kujiunga na Mkataba wa Maji wa Umoja wa Mataifa

Kama nchi ya mkondo wa kati na chini, ushirikiano wa maji yanayovuka mipaka ya nchi ni muhimu kwa Namibia na usalama wa maji wa eneo hilo.
Afrika Upya: 
12 June 2023
Na: 
Fresh water spring in a canyon at Palmwag, Kunene Region, Namibia
Ulrich Doering / Alamy Stock Photo
Chemchemi ya maji safi kwenye korongo huko Palmwag, Mkoa wa Kunene, Namibia.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 
Sauti iko kwa Kiingereza.

Namibia ni nchi ya kwanza Kusini mwa Afrika, na nchi ya 8 barani Afrika, kupitisha Mkataba wa Ulinzi na Matumizi ya Mifumo ya Maji inayovuka Mipaka ya Nchi na Maziwa ya Kimataifa ().

Nchi ya Namibia iliyo na wakazi wapatao milioni 2.5, inashiriki mito yake yote ya kudumu na nchi jirani pamoja na hifadhi kubwa za maji ya chini ya ardhi yanayovuka mipaka ya nchi.

Kama nchi ya mkondo wa kati na chini, ushirikiano wa maji yanayovuka mipaka ya nchi ni muhimu kwa Namibia na usalama wa maji wa eneo hilo na maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.

Waziri wa Kilimo, Maji na Mageuzi ya Ardhi wa Namibia, Bw. Calle Schlettwein alisema: "Ushirikiano kuhusu maji yanayovuka mipaka ni msingi wa usalama wa maji wa taifa letu, na ninaamini kwa dhati kwamba kupitia uridhiaji huu, Namibia haitapata tu faida kubwa kutokana na kushiriki kwake katika mfumo huu wa kisheria ya kimataifa lakini pia itapata fursa ya kuwasiliana na washiriki wenzake katika kuendeleza kanuni za amani na usawa katika kutumia maji yaliyo nje ya mipake yake.

Je, Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji ni nini?
  • Mkataba wa 1992 kuhusu Ulinzi na Matumizi ya Mifumo ya Maji yanayovuka Mipaka ya Kitaifa na Maziwa ya Kimataifa (Mkataba wa Maji), unaojulikana kama Mkataba wa Maji wa Umoja wa Mataifa, ambao sekretarieti yake inahudumiwa na UNECE, ni mfumo wa kipekee wa kimataifa wa kisheria na wa kiserikali.
  • Mkataba huu unahitaji Wanachama kuzuia, kudhibiti na kupunguza athari mbaya kwa ubora na wingi wa maji yanayovuka mipaka ya kitaifa, kutumia maji ya pamoja kwa njia inayofaa na kwa usawa, na kuhakikisha usimamizi wao endelevu kupitia ushirikiano.

"Sheria na kanuni za Mkataba wa Maji zinawiana na sera za Namibia kuhusu ushirikiano wa maji yanayovuka mipaka ya nchi na usimamizi wa pamoja wa rasilimali za maji, tunaposhirikiana pamoja na mataifa mengine kulinda na kutumia rasilimali zetu za pamoja za maji safi".

Katibu Mtendaji wa UNECE, Bi. Olga Algayerova, alisema: "Ninaipongeza kwa moyo mkunjufu nchi ya Namibia kwa kujiunga na Mkataba wa Maji wa Umoja wa Mataifa kama ilivyohimizwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Nchi zote Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Kama Nchi ya kwanza ya Kusini mwa Afrika, Namibia imefungua mlango kwa nchi zaidi katika kanda hii kujiunga na mkataba huu wa kipekee ili kusaidia kukabiliana na changamoto za maji yanayovuka mipaka ya kitaifa, ambayo ni muhimu hasa kutokana na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Baada ya na kuridhia, mapema mwaka huu, huku kunaonyesha umuhimu wa Mkataba wa Maji kama njia muhimu ya kusaidia maendeleo endelevu na kuzuia mizozo juu ya maji ya pamoja,” aliongeza.

Kufuatia Namibia kuridhia Mkataba wa Maji wa Umoja wa Mataifa tarehe 8 Juni 2023, hatua hii itasaidia kuunganisha dhamira ya muda mrefu ya ushirikiano wa maji yanayovuka mipaka ya kitaifa Kusini mwa Afrika.

Namibia imeidhinisha mikataba ya mabonde na ni nchi mwanachama wa mashirika ya mabonde yanayojumuisha: Tume ya Mto Okavango-Cubango (OKACOM) iliyoshirikiwa na Angola na Botswana; Tume ya Mto Orange-Senqu (ORASECOM) iliyoshirikiwa na Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe); Tume ya Njia za Maji za Zambezi (ZAMCOM) na mataifa mengine yote ya kando ya mto kama Botswana, Malawi, Msumbiji, Tanzania, Zambia na Zimbabwe; na Tume ya Njia za Maji za Cuvelai (CUVECOM) na Angola.

Katika ngazi ya kikanda, Namibia ni mshirika wa Mkataba uliorekebishwa wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa mwaka 2000 kuhusu Mikondo ya Maji ya Pamoja na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa 1997 wa Sheria ya Matumizi Yasiyo ya Usafiri kwenye Mikondo ya Maji ya Kimataifa (Mkataba wa Njia za Maji).

Namibia ni moja wapo ya nchi mbili barani Afrika kuwa na vyanzo vyake vyote vya maji safi vinavyovuka mipaka ya kitaifa kusimamiwa na mipangilio ya usimamizi wa uendeshaji kulingana na ripoti ya kitaifa ya uwasilishaji wa zoezi la 2 la ufuatiliaji wa mwaka wa 2020 la Kiashiria cha Malengo ya Maendeleo Endelevu cha 6.5.2, ambacho UNECE na UNESCO ni mashirika. Kwa sasa zoezi hili la tatu linaendelea.

Kama mfumo madhubuti wa kimataifa wa kisheria na kiserikali na jukwaa la ushirikiano na usimamizi endelevu wa maji ya pamoja, yakiwemo maji ya chini ya ardhi, kujiunga na Mkataba wa Maji kunaweza kuwezesha ufadhili kutoka jumuiya ya Wanachama, kubadilishana uzoefu na nchi ya mabonde na nchi duniani kote, kuwezesha upatikanaji wa fedha na ufadhili na kuinua hadhi ya nchi katika ngazi ya kimataifa kuhusu maji yanayovuka mipaka ya kitaifa.

Namibia imeanza majaribio ya miaka miwili , ambayo ni sehemu ya Mkataba huu, kubadilishana uzoefu, kujenga uwezo na kuimarisha ushirikiano wa nchi mbili kuhusu usimamizi wa maji yanayovuka mipaka ya kitaifa. Ni mpango wa kwanza wa Kushirikiana baina ya matifa haya mawili.

Uridhiaji wa wazi na mataifa yote wanachama wa Umoja wa Mataifa tangu tarehe 1 Machi 2016, Mkataba huu sasa una .

Kwa sasa, zaidi ya nchi 20 duniani ziko katika mchakato wa kuridhia, wengi wao kutoka kote Afrika na Amerika Kusini. Nchi 153 duniani kote zinashiriki mito, maziwa na rasilimali za maji chini ya ardhi.

Mkataba wa Maji wa Umoja wa Mataifa unahudumiwa na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi ya Ulaya (UNECE).

Mada: 
More from this author