AV

Wadau wa Usafiri wa Ndege Wawazia Gharama za juu za Usafiri wa Ndege Barani Afrika

Get monthly
e-newsletter

Wadau wa Usafiri wa Ndege Wawazia Gharama za juu za Usafiri wa Ndege Barani Afrika

Sekta ya anga ya Afrika inatafuta njia za kupona baada ya hasara zaidi ya dola bilioni 6 kwa sababu ya kuena kote.
Stephen Ndegwa
10 June 2021
Alfajiri, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cape Town.
Flickr/flowcomm
Alfajiri, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cape Town.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 

Wasafiri wa ndege wa mara kwa mara barani Afrika wanakubaliana kuwa gharama ya tiketi za ndege ziko juu sana.

Mnamo Machi 3, wadau wakuu katika usafiri wa ndege barani Afrika walikutana kwa njia ya mtandao kujadili masuala yanayochangia gharama za juu za usafiri wa ndege na jinsi ya kushughulikia masuala haya.

Katika mkutano huo ulioandaliwa na Kikundi cha Sekta ya Usafiri wa Ndege cha Afrika (AAIG) chini ya mada "Kufikia Usafiri wa Ngege kwa gharama Nafuu barani Afrika," wataalam wa sekta hii walisema kuwa gharama kubwa za safari wa ndege zinatokana na mseto wa masuala yanayojumuisha gharama ya bidhaa zinazouzwa, gharama za michakato ya katikati, ushuru wa serikali, ada ya udhibiti, wakati wa ununuzi (kununua tiketi mapena huwa nafuu), gharama za mafuta, masuala ya soko za mahitaji na usambazaji, na gharama zinazohusiana na Watengenezaji wa Asilia wa Vifaa.

Pia walitambua wasiwasi wao kuhusu usalama na ulinzi, mwingiliano duni barani Afrika, mapungufu ya kufikia soko na miundomsingi isiyofaa kama changamoto zinazokabili sekta hii.

Katibu Mkuu wa Tume ya Usafiri wa Ndege wa Afrika Tefera Mekonnen Tefera alitambua kuwa sekta ya usafiri wa ndege ilikuwa imelemewa zaidi kwa kutozwa ushuru na kulemewa zaidi na ada za juu na gharama na hivyo kufanya kusafiri kwa ndege kuwa na gharama za juu sana katika sehemu nyingi za Afrika.

Bwana Tefera aliongeza kuwa, "Mbali na ada za usafiri wa ndege na ushuru wa serikali, mashirika ya ndege pia hulipa ada zaidi kwa vifaa na huduma za uwanja wa ndege, huduma za kushughulikia nyanja za ndege, usimamizi na huduma za udhibiti na mamlaka ya usafiri wa ndege (CAA).

“Mashirika ya ndege yanakabiliwa pia na gharama za juu za mafuta ya ndege; hata hivyo, ada na ushuru unaotozwa hadi sasa una athari kubwa zaidi kwa bei za tiketi za kusafiri kwa ndege barani Afrika,” alisisitiza.

Gharama kubwa ya mafuta ya ndege

Washiriki katika mkutano huu walilalamika kuwa mafuta ya ndege hugharimu zaidi barani Afrika, hata katika nchi zinazozalisha mafuta yenyewe, kuliko Ulaya au Mashariki ya Kati.

Hali imeboreka sana katika miaka ya hivi karibuni, walikiri, ingawa bado kuna sifa mbaya ya usalama wa mashirika ya ndege ya Afrika ikilinganishwa na maeneo mengine kwa sababu ya masuala kama kuwa na ndege kuukuu, utunzaji duni wa ndege na miundomsingi duni ya nyanja za ndege.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Ndege ya Kenya Gilbert Kibe alisema kuwa gharama kubwa za usafiri wa ndege zimezuia biashara za ndani ya Afrika na za nje, usafiri wa kibiashara na burudani, ambazo zimepunguza ushindani wa bidhaa za Kiafrika katika soko la ulimwengu.

Zaidi ya ada ya anga na ushuru wa serikali, mashirika ya ndege pia hulipa ada na ada ya ziada kwa vifaa na huduma za uwanja wa ndege, huduma za utunzaji wa ardhini, usimamizi na huduma za udhibiti na CAAs (mamlaka ya anga ya umma).

Bwana Kibe alitambua kuwa, "Ukosefu wa mashindano kwa sababu ya ukiritimba wa mashirika makubwa ya ndege kumesababisha kuwepo kwa ndege chache zinazotoza ada sawa na ile ya kusafiri kwenda maeneo ya Uropa."

Mlipuko wa janga la COVID-19 umezorotesha hali ya mashirika ya ndege ya Afrika, kama ilivyo kwingineko ulimwenguni.

Kulingana na Muungano wa Usafiri wa Ndege wa Kimataifa, unaosaidia usafiri wa ndege kwa viwango vya kimataifa vya usalama wa ndege, ulinzi, ufaafu na uendelevu, sekta ya ndege barani Afrika ilipoteza hadi dola bilioni 6 mwaka jana kutokana na janga hili.

Janga la COVID-19 lilizidisha matatizo ya zamani ya usafiri wa ndege barani Afrika kama vile muunganisho finyu baina ya mataifa ya Afrika, masuala ya uchache wa abiria, miundomsingi duni, gharama ya juu ya usafiri ndani ya Afrika, dhamana za juu za fedha.

Ili kurejea, sekta ya usafiri wa ndege imekuwa ikiweka hatua za kuzuia na kudhibiti COVID-19.

Kugharamia mashirika ya ndege ya afrika

Katika mwongo mmoja uliopita, Afreximbank imeadaa zaidi ya dola bilioni 2.5 kufadhili mashirika ya ndege ya Afrika na bado ina hazina inayoendelea ya zaidi ya dola milioni 200, anasema Oluranti Doherty, Mkurugenzi wa Ukuaji na Uuzaji wa nje wa benki hii.

Mashirika mengi ya ndege yamepunguza shughuli zao na wafanyakazi ili kukabili athari za janga hili, gharama ya upimaji wa COVID-19 ikionekana kama ushuru mpya kwa abiria.

Wadau wa sekta hii wanasema kuwa kuanza upya na kurejea kunafaa kutoa fursa kwa usafiri wa ndege barani Afrika kushughulikia gharama za juu ya undeshaji wa shughuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa Crabtree Capital, kampuni ya ushauri wa usafiri wa ndege iliyo na makao makuu Dublin, Mark Tierney, anasema kuwa, "Ikiwa tuna nia ya dhati ya kufanya usafiri wa ndege kuwa wa bei nafuu kwa wengi ili kukuza uchumi na maendeleo, kuna njia mbili tu za kufanya hivyo: ruzuku au kupunguza gharama. ”

Ruzuku hazipo, na hivyo kupunguza gharama ndio njia ya pekee iliyosalia. Ili hili lifanyike, Bwana Tierney anasema kuna haja ya kukomesha kugawanya soko dogo la usafiri wa ndege la Afrika na badala yake kuongeza kasi na upana wa uchumi.

Alitambua kuwa sekta hii inahitaji vifaa maalum kwa mwongozo wa uendelevu na mazoea bora ambayo sekta ya usafiri wa ndege inaweza kutekeleza.

Suluhisho lingine la kupunguza nauli za ndege linaweza kuwa serikali kuingilia kati kwa njia ya utoaji wa ruzuku, ulinzi, kuhusika katika mfumo wa kuongeza thamani haswa ununuzi wa upendeleo wa vifaa muhimu na umiliki wa miundomsingi muhimu na utoaji wa kinga muhimu za kiuchumi.

Taarifa rasmi iliyotolewa baada ya mkutano huo ilisema kwamba, "Hatua zinazofaa zinahitaji kuchukuliwa na sekta ya usafiri wa ndege ili kuimarisha ufanisi wa mashirika ya ndege. Hii ina uwezo wa kupunguza gharama ili sekta ya usafiri wa ndege iweze kufikiwa na kuwa nafuu zaidi kwa idadi pana ya wasafiri kote Afrika. ”

Mada: