¹ú²úAV

Kujumuishwa kwa Wanawake na Haki za Ardhi kama njia ya kuharakisha AfCFTA

Get monthly
e-newsletter

Kujumuishwa kwa Wanawake na Haki za Ardhi kama njia ya kuharakisha AfCFTA

Hatua za pamoja katika mfumo wa vikundi vya wanawake zimewanufaisha sana wanawake katika mazungumzo ya kupata ardhi
Afrika Upya: 
29 December 2023
Kujumuishwa kwa Wanawake na Haki za Ardhi kama njia ya kuharakisha AfCFTA.

Ili kufikia ujumuishwaji na athari za kimaendeleo katika maeneo ya mashambani ya Afrika, pamoja na uendelevu wa mazingira yao, usalama wa umiliki wa ardhi ni muhimu.

Huku ikiwa wazi kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya uzalishaji, biashara na ukuaji wa uchumi – swali linalojitokeza mara kwa mara katika Mkutano wa hivi karibuni kuhusu Sera ya Ardhi katika Afŕika ni, je, inamaanisha nini katika masuala ya ubadilishanaji na mpito – hasa kwa wanawake.

Ardhi ni mali muhimu, ambayo huwezi kuwa na uwezo wa uthabiti wa kiuchumi, mazingira au kijamii bila. [Usalama wa umiliki wa ardhi ni haki ya watu binafsi na vikundi kulindwa dhidi ya kufukuzwa kwa lazima kutoka kwa ardhi yao na serikali. Umiliki unaweza kuwaÌýHuru, Ukodishaji, wa Masharti, Pamoja, au Jumuiya].

Sambamba na ardhi kuna umiliki - kwa namna yoyote ile unafanyika (rasmi au kimila), iwe katika suala la utambuzi wa upatikanaji au umiliki - uwazi wa umiliki ni muhimu katika kuchochea uwekezaji na kuwaruhusu wanawake na walio hatarini kunufaika nao.

Sehemu kubwa ya ardhi barani Afrika bado iko chini ya mikataba ya umiliki wa kimila, ambapo wanaume wanachukuliwa kuwa wamiliki na walinzi wa ardhi.

Ilhali michango mingi inayotolewa katika suala la leba, na maarifa yanatoka kwa wanawake. Kwa hivyo swali ni jinsi ya kuhakikisha kwamba umiliki wa ardhi unawanufaisha wanawake.

Baadhi ya mifano wakati wa mkutano huo imeonyesha faida zinazoweza kupatikana kutokana na hatua ya pamoja katika upatikanaji wa kuwezesha na usalama wa umiliki wa wanawake.

Nchini Uganda na Zambia kwa mfano, utoaji hatimiliki za ardhi wa pamoja kati ya waume, wake na watoto wao huhakikisha kwamba ardhi inabaki ndani ya familia hasa katika matukio ya vifo, hivyo kurahisisha sheria za mirathi.

Aidha, katika mifano mingine, ukodishaji wa ardhi unaofanywa na watu binafsi au vikundi vya wanawake umewanufaisha wanawake na kuonyesha uwezo, hasa katika kilimo hifadhi.

Ukodishaji wa ardhi umeungwa mkono na miongozo inayohakikisha kwamba masuala muhimu yanashughulikiwa mwanzoni na ambayo baadaye, huleta uthabiti wa upatikanaji wa ardhi kwa muda mrefu kwa wanawake.

Nchini Madagaska, mkutano huo ulisikia kuwa wanawake wamekuwa sehemu ya kuchora ramani ya ardhi, ikiwa ni pamoja na ardhi ya jamii ili kujua nini kinapatikana.

Hatua za pamoja katika mfumo wa vikundi vya wanawake ziwameathiri na kuwafaidisha sana wanawake katika mazungumzo ya upatikanaji wa ardhi na kuhakikisha usalama wa umiliki wa muda mrefu, hivyo kuongeza mapato na utoshelevu wa chakula kwa wanawake.

Japo mifano mingi ina umahususi wa kimuktadha, inaonyesha uwezekano wa masuluhisho ya mashinani yanayoweza kuleta manufaa ya muda mrefu kwa wanawake na ambayo yanaweza kusaidia kuongeza tija ya kilimo, upatikanaji wa fedha na masoko.


Annita TipildaÌýni mwanafunzi waÌýShahada ya Uzamili anayechunguza uchumi duara, uendelevu na fursa za kuiga njia mpya za ukuaji wa uchumi barani Afrika katika Idara ya Uchumi wa Chakula na Rasilimali, Chuo Kikuu cha Copenhagen, Denmark.

More from this author