¹ú²úAV

Nishati inayotumiwa upya njia bora kwa mustakabali nyumbufu wa Eritria

Get monthly
e-newsletter

Nishati inayotumiwa upya njia bora kwa mustakabali nyumbufu wa Eritria

Upepo na nishati ya jua baadhi ya nishati nafuu zitumiwazo upya mbadala zilizopo
Afrika Upya: 
17 December 2021
Paneli za jua nchini Eritrea
UNDP Eritrea
Usambazaji wa umeme safi, nafuu na endelevu kwa kaya 8,000 unatolewa kwa Areza na Maidma na vijiji 28 vinavyozunguka vijijini.

Kama mataifa mengine katika Upembe wa Afrika, Eritria haijasazwa na athari mbaya za hali mbaya ya hewa na majanga ya kitabianchi. Sasa ikiwa imekuzwa na zaidi na athari za kijamii na kiuchumi mbazo hazijawahi kushuhudiwa za janga la COVID-19, hali mbaya za tabianchi zinazoongezeka zinahatarisha mwelekeo wa maendeleo wa taifa hilo, kwa kuwa tatizo hilo limedhoofishwa zaidi uwezo wa unyumbufu wa jamii mbalimbali.

Licha ya changamoto hizi, kujiunga kwa Eritria katika mikataba ya kimataifa ya mazingira na nishati ni miongoni mwa juhudi za taifa hilo kubatilisha hali inayoendelea kuwa mbaya ya mielekeo ya tabianchi. Taifa hilo linadhihirisha werevu na kujitolea kwake kwa dhati kwa kuchangia kupunguza utoaji wa gesi ziongezazo joto kwa kuzingatia kanuni msingi za Mkataba wa Paris unaowataka washirika wote kuchangia kikamilifu.

Serikali inatazamia kutimiza lengo lake la kuwajibikia mabadiliko ya tabianchi kwa kuhakikisha mpito wake hadi kwa uchumi usio na kaboni. Inafanya juhudi pia kuongeza kiwango cha uzalishaji wa kawi kutoka kwa nishati inayotumiwa upya.

Bi Amakobe Sande, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Eritrea

Kulingana na Hifadhidata ya Benki ya Dunia kuhusu Ualishi Umeme Ulimwenguni 2019, asilimia 50.3 ya Waeritria wana umeme, huku ualishi wa umeme ukiwafikia asilimia 75.6 na asilimia 36.6 ya wakazi wa mijini na wa mashambani, mtawalia. Ìý

Kutoka kwa makaa ya mawe hadi kwa nishati inayotumiwa upya

unabainisha mabadiliko kutoka nishati inayozalishwa kutokana na makaa ya mawe hadi kwa uzalishaji mseto wa umeme kwa kutumia vyanzo vinavyotumiwa upya na kupunguza hasara za kupitisha na ugavi. Aidha unahimiza teknolojia zinazojali mazingira ili kupunguza utoaji wa gesi zinazoongeza joto duniani. Sekta ya nishati ya taifa hilo pia inasisitiza matumizi na utangulizi wa vyanzo vya nishati inayotumiwa upya kama vile nishati ya jua, upepo na kawi ya mvuke wa ardhini, na kuchukua hatua madhubuti kutoendelea kutegemea makaa ya mawe.

Kupitia kwa NDC wake, Eritria inawazia kuendelea kujitolea kutekeleza hatua za kuingilia kati kupunguza na kurekebisha na hatua muhimu katika mpito wa nishati ili kutimiza mahitaji yanayokua kwa matumizi bora ya nishati na teknolojia za kisasa za nishati.

Bw.James Wakiaga, Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini Eritrea

Serikali inashirikiana na washikadau husika katika sekta mbalimbali kuelekea kupunguza utoaji wa gesi zinazoongeza joto duniani kwa kutekeleza mikondo endelevu isiyotoa kaboni ambazo zinaathiri kupunguza na kurekebika kwa mabadiliko ya tabianchi.

Masuluhisho ya nishati inayotumiwa upya kama upepo na nishati ya jua ni baadhi ya chaguo nafuu zilizopo na ni injini muhimu kwa ubunaji ajira safi na kubuni upya chumi baada ya janga la COVID-19.

Mbali na kuchangia lengo la kutotoa kaboni kufikia 2050, kuongeza upatikanaji wa nishati safi ni muhimu katika kuinua maisha ya jamii kwa njia nafuu, nafuu na endelevu. Kwa hivyo, hatuwezi kupuuza uwezo mkuu wa vyanzo vya nishati inayotumiwa upya ambavyo taifa laweza kuweka ushawishi. Ìý

Hata hivyo, ongezeko la upatikanaji wa teknolojia nafuu linahitajika ili kuhakikisha uwezekano wa kuandama mfuko mpana wa nishati zinazotumiwa upya zinazohakikisha uwezo wa kununua, ufikiaji na urekebu.

Kwa Eritria, fursa muhimu za kuhakikisha nishati safi endelevu ni pamoja na umilikaji ambao serikali na jamii shiriki tayari zimedhihirisha katika kutekeleza miradi ya ufikiaji nishati huku kukiwa na uwezekano mkuu wa kurudufisha na kuongeza.

Tayari jamii zinazitekeleza dhima chochezi kama washirika wa miundo ya kijamii iliyopo ambayo inatoa vyanzo vinavyotegemewa na umiliki ili kupiga jeki utekelezwaji.

Gridi ndogo zinazoendeshwa kwa nishati ya jua zenye uwezo wa kuzalisha megawati 2.25 zinazotoa nishati ya kisasa na nafuu katika miji ya mashambani ya Areza na Maidma kusini mwa taifa hilo na vijiji 33 jirani visivyounganishwa na umeme wa umma ni mfano unaoonyesha jinsi ushirikiano wa sekta ya umma na ya kibinafsi na umilikaji ulivyo muhimu katika masuluhisho ya nishati safi.

Serikali inaweka ushawishi katika vyanzo vya kutumiwa upya na teknolojia kuongeza upatikanaji kwa mwelekeo jumuishi na unaowajali watu ambao unakumbatiwa na jamii yote.

Japo Wizara ya Nishati na Madini inatekeleza mradi wa $ milioni 13 million (Euro 11,762,778) kikamilifu, jamii ilichangia nguvumali na ardhi ya kujenga vituo vya nishati ya jua, na kuongeza uwezo wa matumizi wa mradi huu pamoja na umiliki wa kijamii. Ìý

Ukiwa na Ìýmsaada kutoka Umoja wa Ulaya na UNDP, mradi huu unasaidia zaidi ya watu 40,000 ambao hawakuwa na umeme awali, pamoja na kubuni ajira kwa biashara ndogondogo 513 na huduma zilizoboreshwa katika shule, vituo vya afya na miundomsingi ya nishati utumiwayo upya.

Kuunganisha nyumba na nishati ya jua

Mbali na kuziunganisha nyumba na jamii kwa nishati ya jua, nyumba kadhaa zinazoongozwa na wanawake zimenufaika na kupewa meko yanayotumia nishati kidogo. Haya yanachangia kupunguza matumizi ya mafuta, kupunguza viwango vya uharibifu wa misitu, na kuongeza atahri chanya kwa afya ya wanawake, ikiwa ni pamoja na uhusika wao katika mahitaji msingi ya nyumbani. Ìý

Upatikanaji nishati safi unawezakusaidia kuyaboresha maisha. Hata hivyo, kusawazisha dhrura ya kupunguza utoaji wa gesi na mahitaji mengi ya kiuchumi ni muhimu.

Kwa hivyo, mpito nishati wa Eritria unastahili kuongozwa na njia mbalimbali. Ìý

Ulimwengu u katika kilele cha hatua madhubuti na hatua za dharura za kimaendeleo. Eritria, taifa lenye mchango mdogo sana wa uchafuzi, linaweza kuongoza upatikanaji wa mustakabali salama na endelevu kwa kufuata njia tofauti na mielekeo ya awali ya maendeleo.

Huku taifa hilo likiinuka kutoka katika athari za COVID-19, changamoto kuu sio ikiwa, ila namna, ya kubadili taratibu kuelekea kwa matumizi ya vyanzo vya nishati safi katika kitovu cha ajenda ya mageuzi ya kujenga vyema kuelekea mbele.

Japo zana na mifumo ihitajikayo ipo tayari, taasisi za serikali na washikadau wanastahili kujiepusha na mielekeo ya ubinafsi katika kuzikabili changamoto zinazobadilika za maendeleo na kutumikisha uwezo wa ushirikiano katika sekta zote.

Mkakati wa kitaifa wa ukombozi wa COVID-19 unaweza na unastahili kuwa sehemu msingi ya NDC na mipango ya utekelezi ya tabianchi ya taifa hilo ambayo inasaidia kuongeza kasi ya kujitolea kwake kwa Mkataba wa Paris.

Kwa pamoja, kuna fursa ya kupiga hatua kuu mbele kuelekea kwa mustakabali endelevu, jumuishi, na nyumbufu ambao unalinda walio katika hatari zaidi, na Malengo ya Maendeleo Endelevu yakiwa ruwaza yetu.


Bi. Sande ni Mshirikishi Mkazi wa UN, Eritria, ilhali Bw. Wakiaga ni Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Eritria.

Ìý

Ìý

More from this author