AV

Hakuna aliye salama hadi kila mtu atakapokuwa salama dhidi ya COVID-19 -UN

Get monthly
e-newsletter

Hakuna aliye salama hadi kila mtu atakapokuwa salama dhidi ya COVID-19 -UN

UN News
5 May 2020
By: 
Utafiti wa kutafuta Chanjo ya virusi vya Corona unaendelea
Unsplash
Utafiti wa kutafuta Chanjo ya virusi vya Corona unaendelea

Juhudi kubwa na za kihistoria zinahitajika ili kuweza kulidhibiti janga la mlipuko wa corona auCOVID-19amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo alikuhutubia mkutano wa Muungano wa Ulya wa kutoa ahadi ya kupambana na janga hilo uliofanyika kwa njia ya mtandao mjini Brussels.

Antonio Guterres akatika ujumbe wake amekaribisha mchango wa nchi wahisani kwa ajili ya mfuko wa dola zaidi ya bilioni 8 kwa ajili ya kuongeza kasi ya vipimo, tib ana chanjo ili kutokomeza tishio jipya la virusi vya corona.

Bwana Guterres mara tano ya fedha hizo huenda zikahitajika ili kutuweka sote katika njia ya kuwa huru na gonjwa hilo.

COVID-19 imesambaa kila kona

Hadi kufikia leo hii Katibu Mkuu amesema“COVID-19 imesambaa katika kila kona ya dunia ambapo Zaidi ya watu milioni 3 wameambukizwa ugonjwa huo na wengine Zaidi ya 220,000 wamepoteza maisha.”Guterres ameyasema hayo kufuatia onyo la siku za hivi karibuni kuhusu kutokuwepo mshikamano unaohitajika nan chi zinazoendelea wa kuziwezesha kupambana na janga hili ambalo linasambaa kama moto wa nyika na kushughulikia athari zake kubwa za kiuchumi na kisiasa .

Ameonya kwamba “Zahma zaidi bado inakuja wakati virusi huenda vikashambulia nchi nyingi zenye mifumo duni ya afya.Katika dunia ambayo imeunganika hakuna hata mmoja wetu aliye salama hadi pale wote tutakapokuwa salama”

Ushirika wa kihistoria

Katibu Mkuu ameelezea mkutano huo wa kutoa ahdi ulioanza Jumatatu kama ni kuchukua hatua inayofuata , kukusanya rasilimali kwa ajili ya masuala muhimu. “Nakaribisha ukaribu wa michango iliyotangazwa leo kwa ajili ya lengo letu la awali la dola bilioni 8.2. Fedha hizi ni kianzio kinachohitajika kwa ajili ya kuanzisha nyenzo mpya kwa kasi inayohitajika. Tuna mtazamo mmoja , hebu sasa tutoe kipaumbele kwa watu kila mahali.”

Mkurugenzi mkuu wa

Akiunga mkono yaliyosemwa na Katibu Mkuu katika mkutano huo mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, Dkt. Tedross Adhamon Ghebreyesus amesema kwenye mkutano huo kwamba leo hii viongozi kutoka nchi 40 kote duniani wamekuja Pamoja kuunga mkono ACT kupitia tukio la kimataifa la kuchangisha fedha dhidi ya janga la COVIT-19 , tuki ambalo mwenyeji wake ni tume ya Muungano wa Ulaya.

Ameongeza kuwa“Katika tukio hilo dola bilioni 8.2 zimeahidiwa kwa ajili ya utafiti na utengenezaji wa chanjo, upimaji na tiba. Huu ulikuwa mfano mkubwa na muhimu wa mshikamano wa kimataifa.”

Bwana Tedros ameongeza kuwa leo hii nchi zimekuja Pamoja sio tu kuahidi msaada wa kifedha lakini pia kutoa ahadi ya kuhakikisha kwamba watu wote wanaweza kupata fursa ya nyenzo za kuokoa Maisha dhidi ya COVID-19, kusongesha utengenezaji wa bidhaa zinazohitajika lakini wakati huohuo fursa kuwepo kwa watu wote.

Hata hivyo Dkt. Tedros amesema“Ukweli wa mafanikio hautakuwa tu ni kwa haraka kiasi gani tunaweza kutengeneza nyenzo ambazo ni salama na zinazofanyakazi, lakini itakuwa ni kwa jinsi gani tutakavyoweza kuzigawanya kwausawa. Hakuna hata mmoja wetu atakayekubali dunia ambayo baadhi ya watu wanalindwa na wengine hawalindwi, kila mmoja anapaswa kulindwa.”

Ameongeza kuwa uwezekano wa wkuendelea kwa wimbi la virisi vya Corona duniani kote unahitaji kwamba kila mtu hapa duniani kulindwa dhidi ya ugonjwa huu.

Mbali ya tume ya muungano wa Ulaya ambayo ni muandaaji mkuu wa mkutano wa leo, nchi zmbazo zimehusika kwa juhudi kubwa ni Pamoja na Afrika Kusini, Rwanda, Malaysia, Saudia, Finland na Costa Rica.